Kuna Madhara Kitabibu Kufanya Jimaa’ Wiki Nzima?

SWALI:

 

Assalam Alaykum ninaelewa kua mtu siku na wakati wowote kufanya jima'a ni halali kwa Ahli wake (mke), je kwa upande wa kitabibu nakusudia kiafya haina madhara wiki nzima kufanya jima'i? au kuna limit yake madokta wametuwekea?  mfano ktk wiki mara kadhaa? natumai suala langu limefahamika

 

 


 

 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Tunakushukuru kwa swali lako la kuhusiana na mas-ala ya muda na kiwango cha kufanya jimaa’.

 

Katika Uislamu si kila mas-ala yanajibiwa na Mashaykh au Mamufti bali hutumia ushauri wa wahusikia katika fani unayoligusa suala lenyewe. Ni mfano kama hili suala lako ambalo ulitarajiwa kuelekeza na kuuliza wahusika ambao ni wana fani ya utabibu kwani wao watakutosheleza kwa sababu suala lako ni la kitabibu hivyo unahitaji uwaulize wahusika na sio sisi kwani hapa hatutoweza kukujibu kama unavyotaka.

 

Hata hivyo Maulamaa wanasema kuwa ni wajibu -fardhi- kwa mume kumuingilia mkewe na uchache wake ni mara moja katika kila twahara (baada ya siku zake) ikiwa ataweza, vyenginevyo huwa anamuasi Allaah.

 

Wengine wamesema: Si wajibu kwani ni haki yake; wengine wakasema itampasa kumuingilia mara moja katika kila siku nne kama ilivyothibiti katika kisa cha ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) na mwanamke aliyekuwa akishitaki kuhusu mumewe kuwa haingiliani naye na alikuwepo Ka’b Al-Asad aliyefahamu na kumueleza kuwa amuingilie mara moja katika siku nne. Angalia Fiqhus Sunnah katika mlango wa ndoa.

 

Hata hivyo, unaweza kumuingilia mara nyingi au kidogo uzitakazo kama una uwezo huo na ikiwa ipo haja ya hilo kama mkeo hatosheki mara moja basi unatakiwa umtosheleze hata atosheke.  

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share