Mwezi Kuonekana Baina Ya Nyota Mbili Zilokuwa Ziking’ara Ni Ishara Gani?

SWALI:

 

A.Alykum nimefurahishwa sana na website yenu na Inshallah kutoka saiv nitakuwa najiunga na nitakuwa mwanachama ktk website ALLAh aizidishie wepes zaid. Suala lang:    Hvi karibuni niliona mwezi upo katikati baina ya nyota mbili nyota hzo zilikuwa zkingara cna mpka zkanitia hofu pamoja na mwezi wake ukingara.Ningeliomba kufham kma kuna maana yyte mwezi kuwa katikati ya nyota mbili na kungara kuliko kawaida yke.Kwa sababu cku ya pili nilipoangalia ckuona mwezi kungara cna wala haukuwa ktkt ya nyota zile ambazo mara nyingi huwa karibu na mwezi cjawahi kuziona kukaa katikati zaid ya cku hyo moja.WABILLAH TWAFIQ


 

 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Kwanza kabisa tunapenda kuwakumbusha wote wenye kuzoea kufupisha Salaam au kufupisha kumswalia Mtume wetu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) au kufupisha kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), ni bora waache kufanya hivyo na waandike kwa urefu kwani zote hizo ni 'Ibaadah na ni bora kuzifanya kwa ukamilifu ikiwemo katika kuandika, kutamka n.k. Pia kuongeza neno 'Ta'ala' kwenye Salaam kwa kusema 'Assalaamu 'Alaykum wa RahmatuLlaahi Ta'ala wa Barakaatuh', si jambo tulilofundishwa katika Salaam na hivyo ni bora mtu kuliepuka katika Salaam.

 

.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mwezi kuonekana baina ya nyota mbili.

 

 

Jambo hili mbali na kuwa linaonekana kuwa kinyume na maumbile kwani katika enzi zetu hatujawahi kuona hilo. Hata hivyo, huenda kwa sababu ya kutotaamali kwetu likawa limetokea hata zaidi ya hilo.

 

Tufahamu kuwa hakuna maajabu yoyote kwa hilo kufanyika kwani nyota na mwezi ni miongoni mwa viumbe vya Allaah Aliyetukuka. Na jambo lililokuwa si la kawaida lilitokea wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), naye akaondoa itikadi ambazo zilikuwa zinataka kujitokeza ambazo hazikuwa nzuri.

 

 

Mtoto wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiitwa Ibraahiym aliaga dunia siku ambayo jua lilipatwa. Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) wakaanza kusema kuwa jua limepatwa kwa ajili ya kifo cha Ibraahiym. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawarekebisha Maswahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) kwa kuwaambia kuwa jua ni kiumbe kama viumbe vyengine vya Allaah Aliyetukuka, havipatwi kwa kufa au kuzaliwa kwa yeyote yule.

 

Kwa hiyo, mwezi kuonekana katika hali hiyo na nyota mbili ni miongoni mwa ishara Zake Aliyetukuka haina maana yoyote nyingine. Tayari zipo ishara nyingi sana zinazotufahamisha kuwepo Yeye Aliyetukuka na uwezo Wake.

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share