Imaam Asiyesoma Vizuri Qur-aan Anafaa Kuswalisha?

 

Imaam Asiyesoma Vizuri Qur-aan Anafaa Kuswalisha?

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Swali:

 

Assalamu Alaykum,

 

Imamu ambaye hasomi vizuri Qur-an kiasi ambacho hawezi kusalisha Swala za Jahra (Magharibi, Isha na Asubhi), jee anaweza kutusalisha katika Swala za siri kama vile Adhuhuri na Alasiri?

 

 

Jibu:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuusia kuwa Imaam anatakiwa awe ni mjuzi juu ya wengine kwa kisomo cha Qur-aan. Ikiwa wapo wawili walio sawa kwa ujuzi na elimu ya somo hilo, basi atazamwe aliye mjuzi wa Sunnah za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na ikiwa kwa kipengele hicho pia wapo sawa basi atatizamwa yule ambaye ni mkubwa zaidi kwa umri awe Imaam kama ilivyothibiti katika Hadiyth:

 

  عَنْ أَبِي مَسْعُودٍ الْأَنْصَارِيِّ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((يَؤُمُّ الْقَوْمَ أَقْرَؤُهُمْ لِكِتَابِ اللَّهِ فَإِنْ كَانُوا فِي الْقِرَاءَةِ سَوَاءً فَأَعْلَمُهُمْ بِالسُّنَّةِ فَإِنْ كَانُوا فِي السُّنَّةِ سَوَاءً فَأَقْدَمُهُمْ هِجْرَةً فَإِنْ كَانُوا فِي الْهِجْرَةِ سَوَاءً فَأَقْدَمُهُمْ سِلْمًا وَلَا يَؤُمَّنَّ الرَّجُلُ الرَّجُلَ فِي سُلْطَانِهِ وَلَا يَقْعُدْ فِي بَيْتِهِ عَلَى تَكْرِمَتِهِ إِلَّا بِإِذْنِهِ))  

Kutoka kwa Abuu Mas’uwd Al-Answaariyy (رضي الله عنه)  amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: ((Awaswalishe watu yule mwenye kujua kusoma zaidi Kitabu cha Allaah na wakiwa katika kusoma wako sawa, basi mwenye ujuzi zaidi wa Sunnah, na wakiwa kwenye Sunnah wako sawa, basi aliyetangulia Hijrah, na wakiwa katika hijrah wako sawa, basi mkubwa wao kwa umri,  wala asiswalishe mtu (mwengine) katika nyumba yake wala katika mamlaka yake wala asikae mahali pake pa heshima isipokuwa kwa idhini  yake)) [Muslim]

 

Ikiwa Imaam ni hivyo ulivyosema itabidi mjaribu kutazama aliye mzuri zaidi au ikiwa amechaguliwa na wasimamizi wa Msikiti basi mzungumze na wasimamizi wa Msikiti ili aangaliwe mwengine wa kuongoza Swalaah. Na lau atakuwa hasomi vizuri Qur-aan lakini yeye ndiye bora katika mtaa au eneo hilo, basi huyo ndiye atakayeendelea kuwa Imaam hadi apatikane mwengine.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share