Mashairi: Tamasha Za Ibilisi

 

 

Tamasha Za Iblisi

            ‘Abdallah Bin Eifan (Rahimahu-Allaah)

      Alhidaaya.com

 

Salaam sisi kwa sisi, marafiki na jirani,
Naomba Mola Mkwasi, izidi yetu imani,
Ibada kwa ikhlasi, tuzingatie moyoni,

Atuepushe Manani, Tamasha za Ibilisi.

 

 

Tamasha za Ibilisi, Atuepushe Manani,
Zimeingia kwa kasi, ardhi za Waumini,

Wanaleta unajisi, na tabia za kihuni,
Atuepushe Manani,
Tamasha za Ibilisi.

 

 

Mambo yote ya matusi, yanafanywa hadharani,
Binti hufanywa rahisi, yupo uchi tazameni,
Kama vile sarakasi, huzungushwa hayawani,
Atuepushe Manani,
Tamasha za Ibilisi.

 

 

Waumini wamehisi, ni njama za Wamasoni,

Wamasoni ni kikosi, pamoja na Mazeyuni,

Wameweka majasusi, kutuchunguza nchini,

Atuepushe Manani, Tamasha za Ibilisi.

 

 

Wapo pamoja na sisi, vibaraka mahaini,

Wanatafuta nafasi, kupotoa yetu dini,

Atawashinda Quddusi, Awachape Awala’ani,

Atuepushe Manani, Tamasha za Ibilisi.

 

 

Hawachoki kudadisi, kutaka yenu maoni,

Wapingwe kadamnasi, wakosolewe usoni,

Msiogope polisi, Muogope wa mbinguni,

Atuepushe Manani, Tamasha za Ibilisi.

 

 

“Jahazi la mafarasi,” na “sauti za shetani,”

Ni Tamasha za maasi, poleni wa Kisiwani,

Nia yao ni fulusi, na kukera Waumini,

Atuepushe Manani, Tamasha za Ibilisi.

 

 

Tamasha in kuwaghasi, kupoteza ikhwani,

Na kuwaharibu nafsi, vijana na wanandani,

Ili dini iwe basi, waidharau mwishoni,

Atuepushe Manani, Tamasha za Ibilisi.

 

 

Mungu hulipa kisasi, msidhani Hawaoni,

Mwisho wake ni yabisi, kukauka mashambani,

Madhambi huwafilisi, mwisho in umasikini,

Atuepushe Manani, Tamasha za Ibilisi.

 

 

Kweli nina wasiwasi, ndugu wapo hatarini,

Ombeni dua upesi, Awalinde Rahmani,

Naichana karatasi, nimefika kikomoni,

Atuepushe Manani, Tamasha za Ibilisi.

 

 

 

 

 

Share