Shurba Ya Nyama Mbuzi - 3

Shurba Ya Nyama  Mbuzi  - 3

Vipimo

Nyama ya mbuzi - 2lb

Nyanya - 1

Kitunguu - 1

Kidonge cha supu - 1

Maji - 4 mugs

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha supu

Bizari ya pilau(cumin) - 1 kijiko cha chai

Bizari ya manjano - ½  kijiko cha chai

Mdalasini - 1 kijiti

Shairi (oats) - 5 vijiko supu

Pilipili mbichi - 2

*Siki ya zabibu - 2 vijiko vya supu

Chumvi - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Osha nyama vizuri tia kwenye sufuria.
  2. Katakata kitunguu na nyanya,ikiwa hupendi  maganda ya nyanya toa na ukate kate.
  3. Tia kidonge cha supu, mdalasini, chumvi na maji finika uchemshe nyama mpaka iwive.
  4. Tia shairi (oats)  kwenye bakuli na maji iache, nusu saa kisha isage  kidogo tu, na mimina kwenye supu ya nyama.
  5. Tia pilipili mbichi nzima, thomu, bizari zote na siki. Weka moto mdogo mdogo huku unakoroga kila baada ya muda.
  6. Tazama uzito, na ongeza maji kidogo ikiwa nzito sana

Kidokezo:

Ikiwa huna siki ya zabibu tia ndimu.

 

 

Share