Supu Ya Kuku Na Viazi/Mbatata

Supu Ya Kuku Na Viazi/Mbatata

Vipimo

Kuku - 4 LB

Viazi/mbatata - 3

Kitunguu maji - 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 5 chembe

Pilipili mbichi - 2

Nyanya ya kusaga - 1 kijiko cha chai

Pilipili manga ya unga - ½  kijiko cha chai

Haldi/tumeric/bizari ya manjano - ¼  kijiko cha chai

Mafuta ya zaytuni - 2 vijiko vya supu

Kotmiri (coriander freshi) - 1 msongo

Ndimu/siki - 2 vijiko vya supu

Chumvi - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Osha kuku na ukate vipande vipande kiasi
  2. Menya viazi/mbatata, katakata vipande kiasi.
  3. Menya kitunguu maji ukate vidogodogo
  4. Weka mafuta katika sufuria, kisha tia vitunguu vikaange kidogo tu hadi viwe laini.
  5. Kisha  tia vipande vya kuku, chumvi, pilipili manga, thomu ilochunwa (grated) au kukatwakatwa vipande vidogodogo.
  6. Tia nyanya,  haldi, na maji kiasi.
  7. Tia viazi/mbatata na iache ichemke hadi kuku na viazi/mbatata ziive.
  8. Katakata kotmiri na pilipili mbichi ndogo ndogo utie mwishoni.
  9. Tia ndimu au siki ikiwa tayari kuliwa  na mkate au upendavyo

 

 

 

Share