Dhokra
Dhokra

Vipimo
Unga wa mahindi au wa mchele - ¼ magi
Unga wa dengu - 2 magi
Mtindi (yogurt) - 1 kopo
Manjano - 1 kijiko cha supu
Kitunguu saumu (thomu/galic) - 2 vijiko vya supu
Pilipili ya chupa ya Sambal - 2 vijiko vya supu
Chumvi - 1 kijiko cha supu
Sukari - 6 vijiko vya supu
Pilipili mbichi - upendavyo
Kotmiri - kiasi
Baking powder - 1 kijiko cha chai
Ndimu - 1
Rai - 2 kijiko cha supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Changanya yogurt, unga wa mahindi na unga wa dengu vizuri
 - Kata vitunguu, kotmiri, na pilipili mbichi vipande vidogo.
 - Kisha uchanganye na vipimo vilivobaki isipokuwa baking powder
 - Paka kisinia kidogo mafuta tia mchanganyiko kwenye bakuli kiasi
 - Tia baking powder changanya kisha tia kwenye kisinia uliyoitayarisha.
 - Chukuwa sufuria kubwa kidogo tia maji kikombe kimoja kisha weka bakuli jengine ndani ya sufuria ya maji.
 - Tia kisinia cha mchanganyiko juu ya kibakuli funika vizuri upike kwa mvuke (steam) muda wa saa hivi.
 - Weka mafuta Kijiko kimoja cha chai kwenye kisufuria kidogo ukaange rai kotmiri na pilipili mbichi.
 - Ikishaiva dhokra utanyunyiza kwa juu pamoja na masala ya unga
 - Kidokezo
 - Unaweza kuweka kwenye friji ukafanya kidogo kidogo
 
    
    