Sambusa Za Kuku Na Mboga

VIPIMO
Manda ya sambusa ya tayari Kiasi inavyouzwa
(Kiasi ya sambusa 40-50)
Mafuta ya kukaangia Kiasi
Kuku (kidari) kilichosagwa 1 Kilo
Thomu na tangawizi iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 Kijiko cha chai
Pilipili manga 1 kijiko cha supu
Bizari ya pilau ya unga (cummin powder) 1 kijiko cha chai
Bizari ya mchuzi 1 kijiko cha chai
Ndimu 1 kijiko cha supu
Mboga mchanganyiko (za barafu) 1 kikombe
Chumvi Kiasi
Nyanya iliyokatwa ndogo ndogo 1
Vitunguu maji vilivyokatwa (chopped) 1 Kikombe
Kotmiri iliyokatwa (chopped) 1
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Pika nyama ya kuku ya kusagwa kwa kutia chumvi, thomu na tangawizi, pilipili, ndimu na bizari zote.
2. Karibu na kuwiva tia mboga za mchanganyiko (frozen vegetables).
3. Zima moto na tia nyanya, vitunguu na kotmiri.
4. Funga sambusa katika manda
5. Pika sambusa katika mafuta ya moto hadi ziwe nyekundu na zikiwa tayari kuliwa.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
