Katlesi Za Mviringo Za Samaki

Katlesi Za Mviringo Za Samaki 

Vipimo

Viazi - 7-8 kiasi

*Samaki wa Tuna wa kopo -  3 vibati

Kitunguu - 1

Chumvi - kiasi

Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai

Pilipili mbichi - 1

Ndimu -  1 kijiko cha supu

Kotmiri (Corriander leaves) - ½ kikombe

Unga wa ngano - ½ kikombe

Chembe za mkate  (Bread crumbs) - 1 kikombe

Mayai - 2

Mafuta ya kukaangia - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Chemsha viazi hadi viwive, menya na uviponde uweke kando.
  2. Katakata kitunguu,  pilipili mbichi, kotmiri ndigo ndogo (chopped) weka kando.
  3. Tia tuna katika kikaangao (frying pan), mchanganye na chumvi, pilipili manga, pilipili mbichi, kitunguu na ndimu kisha weka motoni mkaushe akolee viungo hivyo.
  4. Epua tia kotmiri uchanganye vizuri.
  5. Chukua kiasi cha viazi viliyopondwa ufanye kiduara mkononi na utie mjazo wa tuna.
  6. Kisha chukua tena viazi kiasi kidogo ufunike huku unatandaza viazi na kufanya duara kama ya picha. Endelea hadi umalize viazi na mjazo weka kando.
  7. Weka unga wa ngano katika sahani pekee. Weka chembe za mkate (Bread crumbs)  katika sahani nyingine na piga yai katika sahani nyingine.
  8. Chukua donge la viazi ulojaza, chomva katika unga, kisha katika yai, kisha katika chembe za mkate,   kisha uchome katika karai au kikaango.
  9. Zitakapobadilika rangi, epua weka kando zikiwa tayari.

Kidokezo:

Unaweza kutumia samaki wa nguru badala ya tuna ila itabidi umtie  maji kidogo apikike vizuri hadi akauke.   

 

 

 

 

Share