Anasomewa Kwa Kutumiwa Kombe Na Kutafsiriwa Ndoto Zake, Inafaa?

SWALI:

 

Asalam aykum waramatullah wabarakatu

Nakuombeni munisaiodie haraka vile mutaweza. ....... kampigia mtu ambae anasomea watu na kutumia makombe kama una matatizo, sasa kabla kumwambia chochote kamwambia ampe jina lakena la mama yake halafu atamwambia matatizo yake. Sasa anavyosema yule mwanamke kuwa anasoma linakuja jina la nabii sasa ndio inakua ndoo nyota ya .........

kama vile yule nabii yalovyopata ndoo na yeye tapata je nikweli? Kamwambia anafanyiwa ubaya na ataelekea  ginigi je ni kweliiiiiii? Hana raha ....... analia tuu tangu kaambiwa, mimi mwembia subiri nikuulizie kwanza halafu ndo utamfata huyo bibi akuzinguwe na akupe makombe, nakuombeni munijibu haraka vile mutaweza ........hana raha analia tuu hajuii hafanye nini


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kufanyiwa kombe na kutafsiriwa ndoto.

 

Hakika hakuna tatizo kutafsiri ndoto kwa aliye mjuzi wa hilo. Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitafsiri ndoto na hata Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) alifanya hilo. Na tabii‘, Ibn Siiriyn alikuwa anatafsiri ndoto.

 

Hata hivyo, baada ya kusoma swali lako inaonyesha huyo mliokwenda kwake si mjuzi kabisa bali yeye ni mganga tapeli, mpiga bao au mnajimu kwani ndivyo wanavyofanya kwa kutazama mikono au kuuliza majina ili waweze kutazamia kwa kupitia njia ambazo si za sheria ya Kiislamu.

 

Ushauri wetu ni kuwa umpeleke mgonjwa huyo kwa Shaykh wa Sunnah ambaye atamtibu kwa njia za shari’ah na huku naye (mgonjwa) akijaribu kujitibu kwa kusoma Qur-aan kila wakati pamoja na adhkaar zilizosuniwa na shari’ah.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share