SWALI:
Assalaam Aleikum,
Je inafaa kufanya kazi ya kupiga video maharusi au sherehe zinazo husisha wanawake kuto kujisitiri kulingana na sheria ya kislamu. Naomba Muongozo.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Asli katika upigaji picha iwe ya kawaida au hata ya video ni haramu isipokuwa picha za dharura kama vile picha za passport na zenye kufanana na hilo kulingana na dharura iliyopo au itakayokuwepo; na harusi si jambo la dharura wala haliwezi kuingia katika dharura kwa hali yoyote ile na pia maziko ambayo yamekuwa yakichukuliwa kwa video.
Ingia kwenye viungo vifuatavyo uweze kusoma kuhusu hukmu ya picha:
Hukmu Ya Kuchora Au Kupiga Picha Za Viumbe Vyenye Roho
Malaika Hawaingii Nyumba Iliyotundikwa Picha Za Familia?
Muislamu hatarajiwi kuwa kazi yake ya kumpatia riziki ya halali kuwa ni kazi yenye uharamu zaidi kuliko uhalali.
Haijuzu kwa hali yoyote ile kuwachukua video au kuwapiga picha maharusi au kumfunua biharusi mbele ya waliohudhuria sherehe ya harusi hata akiwa na mumewe pamoja naye; bali inalazimika kwa biharusi kujisitiri na kuwa mbali na wanaume wasiokuwa maharimu wake na hasa hasa ‘masheikh’ wenye kudai kuwa wanaingia chumbani kumsomea du’aa na wale wenye kujipachika jina la ‘best man’.
Pia haijuzu kuwachukua picha wanawake waliohudhuria sherehe ya harusi au nyenginezo wawe wamejisitiri au vyenginevyo hali zote ni sawa sawa.
Ikiwa hali ndio kama hii basi mchukuaji picha au video huwa yuko hatarini kwa kazi yake kwani huwa bila ya shaka yoyote ile anafanya haramu; haramu yenyewe ina vipengele vingi baadhi yake ni
Uharamu wa kumuangalia mwanamke/wanawake asiye/wasiokuwa maharimu wake kwa macho yako ya kawaida tena kwa makusudi achilia mbali wakati huo huwa anatumia kifaa chenye uwezo wa kumvuta karibu na kumuona mengi zaidi usiyoweza kuyaona kwa macho yako.
Na isitoshe wenye kufanya hivyo, huenda kwenye studio zao, au majumbani kwao na kuzitengeneza na kuziunganisha hizo video, huku wakizitazama na wanaume wengine wasio Mahram wa hao wanaotazamwa, na zaidi pia, huenezwa video hizo sehemu mbalimbali wakaona wengi na fitna ikatapakaa na uovu kuzidi.
Qur-aan inasema:
"Waambie Waumini wanaume wainamishe macho
Uharamu wa kuchanganyika yeye na wanawake wasio maharimu zake hata
Uharamu wa kuwa utakuwa unafanya yaliyokatazwa wazi na kujichumia majidhambi bila ya wewe kuelewa na kufanya tendo
“Atakayefanya kitendo chema katika Uislam atapata ujira wake na ujira wa yule atakayekitenda baada yake bila ya kupungukiwa thawabu zao. Na atakayetenda kitendo kibaya katika Uislam atabeba (mzigo wa) dhambi zake na dhambi za yule atakayetenda wala hapungukiwi kitu katika (mzigo wa) dhambi hizo.” (Muslim)
Uharamu wa kujichukulia nasibu yako -sehemu- yako katika zinaa; kwani Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Hakika Allaah (‘Azza wa Jalla) amemuandikia mtoto wa Aadam fungu lake katika zinaa ambalo halikwepeki, jicho linazini na zinaa yake ni kuangalia, na ulimi unazini zinaa yake ni kutamka, na nafsi zinaa yake ni kutamani, na kadhalika utupu husadikisha au hukanusha...)) (Imepokelewa na Al-Bukhaariy, kitabu cha ‘Idhni’. Mlango wa ‘Zinaa ya viungo visivyokuwa utupu/uchi.’)
Ameanza na zinaa ya jicho na wewe ndio kazi yako ya kila siku au karibu kila pakiwa na harusi au sherehe ze mchanganyiko; na wewe huwa katika makuwadi -samahani sio neno zuri lakini hakuna jengine zaidi ya hilo kwani wanaume wenye kutazama hiyo/hizo video huwa ushawafanyia kazi kubwa na kuwafanyia wepesi wa kuwaangalia wanawake; bila ya video yako wasingepata wepesi huo kwani wengine huwa hawaonekani isipokuwa katika video zako.
Hivyo, hiyo sio kazi ya kufanya, ni kazi yenye uharamu na ufisadi mwingi, jaribu kujiepusha nayo na kuomba maghfirah kwa yaliyopita na kutafuta kazi nzuri ya halali kuifanya.
Na Allaah Anajua zaidi