Anataka Dalili Ya Kuwa Maimamu Wa Kishia Wanajipangia Wenyewe Kufa

 

Anataka Dalili Ya Kuwa Maimamu Wa Kishia Wanajipangia Wenyewe Kufa

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

  

Asalamun alaykum

Nashukuru kuhusu lile suali  langu la kuhusu mashia kuwatukuza maimam lakini mm nimesomakam hivyo mlivyosoma nyinyi kuhusu hivyo vitabu vya kishia lakini  hayo  mmsijaoyaona sasa sijui  nyinyi  mmeyatoa wai  na vile vile mnasema  eti maimam  hua wanajipangia wenyewe siku ya  kufa mm hiyo sijaona naomba mnipatitie hicho kitabu  kwani  mm  huwa nakwenda huko  iran mara kwa mara lakini pia  nimefuatilia saan mambo hayo lakini sijayaona na hata kua mnasema  kua huyo Abdullah bin Sabaa ndie alienzisha huo ushia mm nimefanya tahkiki huku huku iran  lakini sio kweli  na nilisoma kitabu kilichoandikwa ujue ushie na nimesoma  kwa vizuri tu lakini pia wao mwenyewe wanakanusha sasa wai niwakubali  nyinyi au mashi naomba mkinijibu masuala  yangubasi fanyeni tahkiki  kwa uzuri zaidi  kwani hatamnaweza pengine  kuongeana shia  mwenyewe sasa  sijui mtafanya  nini? Wa aleikum msalam salam kotoka znz.

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Hii hapa chini ni dalili na nyingine za ziada kwa faida:

 

1.    Imam anajua wakati wa kifo chake na anachagua anavyotaka kufa (anakufa kwa kutaka kwake). [Usool-ul-Kaafi, Mjalada 2, Ukurasa 23, Iliyochapwa huko Iran]

 

Pia pokea na hizi nyongeza za kufru na upotofu uliomo kwenye hivyo vitabu vya Kishia.

 

2.    Imamu wana elimu zaidi ya Rusuli (ina mapokezi zaidi ya 13) [rejea Bihaar al-Anwaar, mjalada wa 26, ukurasa wa 194 hadi 200]

 

3.     Imamu ni wajuzi kuliko Rusuli, Manabii na vyote vilivyoumbwa. Rusuli wakubwa Nuwh, Ibraahiym, Muwsaa na ‘Iysaa wamepata daraja ya Uwlul-‘Azm kutokana na kuwapenda Maimamu [ina mapokezi 88]

 

4.     Dua za Rusuli na Manabii zilijibiwa kwa sababu walizipitishia kwa Maimam [ina mapokezi 16]

 

5.   Imam wana uwezo wa kufufua wafu. Wanaweza kutibu Upofu na Ukoma. Wana Elimu walizopewa Rusuli na Manabii [ina mapokezi 4]

 

6.   Hakuna Elimu ya Mbinguni, Ardhini, Peponi na Motoni iliyofichwa kwao. Walioneshwa Ufalme wa Mbinguni na Ardhini. Wanajua yote yaliyotokea na yatakayotokea mpaka Siku ya Qiyaamah [ina mapokezi 22]

 

7.    Imamu wanajua ukweli wa Imani ya Mtu au Unafiki wake. Wanacho kitabu cha Majina ya Watu wa Peponi, Majina ya Wafuasi wao na Maadui zao [ina mapokezi 40]

 

Kutokana na Sifa na uwezo wa Imamu wa Kishia inaonekana kwamba, wao sio Watawala au viongozi wa Kiroho tu bali wao pia ni wana uwezo na sifa kama za Rusuli na Manabii na licha ya yote dunia inawategemea kwa kila hali na kwa kuthibitisha haya Khomeini ameandika nadharia hii nzima kwa kuhalalisha mapinduzi katika kitabu chake Al-Hukumat al-Islamiyah.

 

8.  “Ni nguzo ya Imani yetu isiyopingika kwamba Imamu wetu wana vyeo mbele ya Allaah ambavyo Malaika na Rusuli wanavitamani” (rejea kitabu hicho ukurasa wa 52)

 

 

Hayo kwa uchache ni upotofu na ukafiri uliojaa kwenye vitabu vya Kishia. Na unaweza kuvitafuta vitabu vyao hivyo kama:

Usuulul Kaafi

Man La Yahdhurul Faqiyh

Al-Istibsaar

Wasaail Ash-Shiy’ah

Bihaarul Anwaar

Kashful Asraar

Faslul Khitwaab Fiy Tahriyf Kitaabi Rabbil Arbaab

Haqqul Yaqiyn

Al-Hukuumat Al-Islaamiyah

 

Na vingi vinginevyo ambavyo utaona ndani ya vitabu hivyo.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

Share