Labania Za Maziwa

Labania Za Maziwa

 

 

Vipimo
 

Maziwa ya unga -  2 vikombe

Sukari -   3 vikombe

Maji  - 3 vikombe

Unga wa ngano - ½ kikombe

Mafuta  - ½ kikombe

Iliki -  kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Paka sinia mafuta kabla ya kupika labania
    Katika sufuria chemsha maji na sukari pamoja na iliki mpaka inate vizuri 
  2. Kisha mimina  mafuta koroga 
  3. Halafu mimina unga wa ngano na ukoroge haraka haraka 
  4. Kisha tia unga wa maziwa, endelea kukoroga usiwe na madonge mpaka uwe rangi ya  browni isiokoleza. 
  5. Kisha mimina  mchanganyiko kweye sinia uliyoipaka mafuta, iwache ipoe  na kata kata upendavo na itakuwa tayari.

Kidokezo:

Katika vipimo ni vizuri utumie kikombe cha kupimia (measuring cup)

 

 

 

Share