Mitai-2

Mitai 2

 

 

Vipimo

 

Unga wa ngano - magi 2 (vikombe vikubwa)

Hamira  kijiko 1 cha chai

Sukari Vijiko 2 vya supu

Maziwa  ¾ Magi

Siagi Vijiko 2 vya supu

Mafuta ya kukaangia kiasi

 

Shira

Sukari  ¾ Kikombe

Maji  ¾ Kikombe

Illiki ya unga kiasi

Zafarani kiasi

 

Namna Ya  Kutayarisha Na Kupika

  1. Katika bakuli, changanya vipimo vyote pamoja na ukande unga usiwe mgumu wala laini sana uwe kiasi.
  2. Kisha fanya donge moja na iache pahali penye joto mpaka iimuke.
  3. Halafu weka mafuta ya kukaangia kwenye moto.
  4. Sukuma donge hadi liwe duara sio nyembamba sana, kisha katakata kama ilivyo kwenye picha.
  5. Mafuta ya kisha pata moto choma mittai hukuunazigeuza hadi ziwive na kugeuka rangi.
  6. Katika sufuria tia vipimo vya shira na iache ichemke isiwe nzito sana.
  7. Mimina mitai kwenye shira na uzipepete, kisha weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

Share