Buns Tamu Za Ufuta Na Malai Chungu (sour Cream)

Buns Tamu Za Ufuta Na Malai Chungu (sour Cream)

Vipimo

 

Unga - 4 Vikombe

 

Sukari -  1 Kijiko cha supu

 

Chumvi - 1 Kijiko cha chai

 

Hamira - 1 Kijiko cha supu

 

Baking powder - 1 Kijiko cha chai

 

Siagi - ¼ Kikombe

 

Maziwa -  1 ½ Vikombe

 

Malai chungu (sour cream) - 2 Vijiko vya supu                                 

 

Ufuta - Kiasi ya kunyunyizia juu

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Katika bakuli changanya vipimo vyote isipikuwa ufuta.
  2. Kisha ukande unga huku unanyunyizia unga ukiwa unashika.
  3. Funika mchanganyiko na weka pahali penye joto hadi iimuke.
  4. Halafu fanya viduara na viweke kwenye treya ya kuchomea iliyopakwa siagi.
  5. Ziache pahali penye joto hadi zimuuke kwa mara ya pili.
  6. Washa oveni moto wa 350°.
  7. Pakiza (brush) Yai uliopiga au maziwa juu ya vile vidonge kisha nyunyizia ufuta juu.
  8. Kisha vumbika kwenye oveni kwa muda wa dakika 15 hivi na kuweka moto wa juu hadi ziive na kugeuka rangi na zitakuwa tayari kuliwa.
Share