Mkate Wa Nyama

 Mkate Wa Nyama

 

Vipimo

Nyama ya kusaga -  ½ LB

Kitunguu maji kilichokatwa kidogo - 1

kidogo (chopped)

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagawa - 1 Kijiko cha chai                   

Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai

Unga wa ngano-  2-3 vikombe

Hamira - 1  au  1½ kijiko cha chakula 

Chumvi -  ½ kijiko cha chai

Mayai -  5

Siagi -  225g

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Tia katika nyama thomu, tangawizi, chumvi, pilipili manga, (ukipenda bizari zako nyingine), vitunguu, kisha iache kama muda wa saa moja ili vikolee hivyo vitu kwenye nyama.
  2. Ikaushe nyama  mpaka iwive kama nyama ya sambusa.
  3. Vunja mayai manne na la tano liache pembeni. Yatie kwenye bakuli upige kama kiasi cha dakika mbili.
  4. Tia unga kwenye mayai na changanya vizuri kisha tia hamira na chumvi halafu changanya kwa sekunde chache tu.
  5. Halafu tia siagi kwenye bakuli la unga na uchanganye vizuri mpaka uchanganyike vizuri yaani lifanyike donge halafu uzunguushie karatasi ya plastiki (plastic wrap) au mfuko wa plastiki, na uweke kwenye friji kwa usiku mzima ulale yaani ni vizuri ulale siku nzima ili ladha yake itokeze.
  6. Siku ya pili toa unga kutoka kwenye friji na uweke kwa muda wa saa moja ili ukande kwa kutumia siagi na lile yai moja lililobakia mpaka uwe laini.
  7. Sukuma kwa kifimbo kama unataka kufanya chapati, yaani utandaze kwa kifimbo halafu ukishakua bapa (flat) chukua nyama yako itandaze juu ya ule mkate yaani nyunyiza kwenye ule unga ulioutandaza.
  8. Kunja unga (roll)  na nyama yake ukisha unauzunguusha duara ili kuutia kwenye treya yako ya kubake unauacha uumuke.
  9. Ukishakuumuka unapaka siagi au yai juu yake ukisha unaupika katika jiko (oven) kama unavyopika mikate mengine kwa moto wa 350 Deg. Na kwa muda wa kama dakika 20 au zaidi hadi uwive.

Kidokezo

Ni vizuri kuliwa kwa  chai au juice

 

Share