Amemuacha Mke Mkubwa Kwa Wazazi Wake Ambako Hakuna Masikilizano – Mume Hamdumii Je Ana Haki Kudai Talaka?

SWALI:

 

Assalam alaikum warahmatullahi wabarakatu...........

 

Natumai muko wazima wa afya alhamdullilah.....niko na swali ningefurahi kupata majibu.

 

Wewe ni mwanamume ulie owa mke wako na uka muweka aishi na mama yako wazazi kwa muda wa miaka mingi kama kumi na saba hivi sababu wewe unafanya kazi nchi nyengine ...wewe huleti chakula wala maangalizi ya mke wako na wanao na sasa mkeo amevumilia mambo madogo madogo na pia upuuzi ambao anafanyiwa kwenu maana nyumba anayoishi ni ya jamii kuna dada zako na kaka zako pia mpaka anataka kuishi pekee na watoto wake. Je huyu mke anayo haki ya kuishi pekee ama ni mpaka mama yako aridhike ndio umpe mkeo nafasi ya kuishi maisha yake na watoto wake. Sababu kubwa ni huyu mwanamume anataka kumkalisha mkewe na mamake wapate kusuluhisha hitilafu baina yao na mke hataki je huyu mke afanye nini? na huyu mume tayari  ameshaowa wake wengine wawili na kila mke anaishi kwake na mke mkubwa bado yuko kwa wazazi wake mume na hakuna uadilifu wowote huyu mume anaofanya na ukimwambia ni kelele na kuwa yeye anajua zaidi kwa kuwa ni mume utafanya vile anataka..........tafadhali muelezeni huyu bibi afanyeje?

         

 

mimi nimeolewa muda wa miaka 17 na naishi na wazazi wa mume wangu.....Miaka kama minane ya kwanza tulikuwa tunaishi vizuri halafu kukatokea hitilafu kidoga baina ya yule mama na mimi nkaenda kwetu nyumbani kumchukuwa mama yangu ili tupate kusuluhisha hio hitilafu  lakini mavya yangu alikataa kata kata kusikiza bali aliniambia miende zangu hanitaki nyumbani kwake ......wakati nikiolewa mume wangu alikuwa ni mtu wa safari mpaka hii leo. Ajabu ni kuwa mume wangu alikataa kusikiliza upande wangu bali alisikiliza upande mmoja tu wa mama yake..........alitaka niende kumuomba mama yake msamaha kwa kosa ambalo sijafanya na maneno mengine mingi mama yake alisema.....niliishi kwetu kwa muda wa miezi 8 alikuwa haniangalii kwa chochote bali alikuwa akinipigia simu ili niende niombee msamaha. Baada ya miezi 8 niliamua kuenda kuomba msamaha nikarudi kwao kwa ahadi ya kuwa baada ya miezi 3 au 4 tutagura tuishi pekee yetu, mpaka hii leo ahadi bado haijatimizwa na mume ashaowa wake wengine wawili na kila mtu anaishi kwake........sasa nifanyeje


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuweka katika nyumba ya mkwe wako. Hakika ni kuwa mke ana haki ya kuomba kutoka kwa mume wake kuajiriwa nyumba akaishi yeye, mumewe na watoto wao. Na njia hiyo pia inaondoa fitna nyingi zinzotokea baina ya mama na dada za mume kama ulivyoeleza.

 

Kwa hali hiyo ulivyo sasa, ni wewe kufanya yafuatayo:

 

  1. Kuondoa tatizo hilo ni kuzungumza na mumeo kwa njia nzuri akuruhusu uende kwenu mpaka atakapo rudi nyumbani muweze kulizungumza suala hilo. Na lau kama atarudi karibuni basi vumilia mpaka atakapokuja ili mzungumze hilo kama wanandoa na watu wazima wenye busara.

 

 

  1. Ikiwa jambo hilo la kwanza limeshindikana basi itisha kikao baina yako, mumeo, wazazi wake na wako au wawakilishi wenu ili mzungumzie suala hilo mpte kulitatua.

 

 

  1. Ikiwa hakukupatikana ufumbuzi wowote peleka malamishi yako kwa Qadhi ambaye atawasikiliza nyote wawili na kuamua kulingana na utakavyo Uislamu.

 

Ufahamu kuwa kama mke unao haki kwa mumeo kukupatia makao, lishe, matibabu na mengineyo katika mambo ya kimaisha.

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

Share