Kufunga Swawm Za Sunnah Kuanzia Ijumaa Inafaa?

 

Kufunga Swawm Za Sunnah Kuanzia Ijumaa Inafaa?

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Assalam Aleikum. Nina swali langu moja je nikita kufunga swawm (suna) nikianza siku ya ijuma inawezekana noamba muni jubu hili sawali Allah Awazidishie elimu.

 

 

JIBU:

 

 

 AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

  Tufahamu kuwa Ijumaa ni siku kuu yetu ya kila wiki. Kwa ajili hiyo haifai kuihusisha haswa siku hiyo ya Ijumaa kwa funga isipokuwa ikiwa ni siku maalumu ya Sunnah kama siku ya ‘Arafah, ‘Aashuraa’ na siku nyenginezo. Ama mbali na siku hizo haifai kufunga Ijumaa peke yake.

 

Njia moja ambayo inakuwezesha wewe kufunga siku ya Ijumaa ni ima kufunga Alkhamis, kisha ukafuatisha na siku ya Ijumaa au ufunge siku ya Jumamosi baada ya Ijumaa. Hii ni kwa mujibu wa Hadiyth ya Juwayriyah bint al-Haarith (Radhwiya Allaahu ‘anhaa): Nabiy (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) alimtembelea (yeye Juwayriyah) siku ya Ijumaa, naye alikuwa anafunga. Alimuuliza: “Je, ulifunga jana?” Nikajibu: “La”. Akasema: “Je, una niya ya kufunga kesho?” Nikasema: “La”. Akasema: “Basi fungua swawm yako” (al-Bukhaariy).

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Hukmu Ya Kufunga Ijumaa Ikiwa Ni Siku Ya 'Arafah Au 'Ashuraa

 

Hukumu Ya Kufunga Siku Ya Jumamosi Pekee

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

 

Share