Kwa Nini Wanaume Wana sehemu Kubwa Zaidi Ya Kurithi Kuliko Wanawake?

SWALI:

 

Asalam Aleykom  

mimi  nimeletewa  website yenu  na shukuru sana, Swali ni hii: panda kujua kwa nini  mwanamke  ana rithi  asilimia 25% kuliko  mwanamme  anarithishwa  aslimia 75%?    maa na mwana ume anaweza kuharibu  mali ya kuridhi kwa njia mbaya kuliko mwanamke?

 


 

 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kwa nini mwanamme anarithi fungu zaidi kuliko mwanamke.

Mwanzo inafaa tufahamu kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Hapitishi jambo ila lina manufaa ya mwanaadamu kwa jumla. Baada ya hapo inatakiwa tufahamu kuwa mwanamme harithi mara tatu ya mwanamke kama alivyoandika muulizaji. Urithi unagawiwa kulingana na alivyotaka Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na warithi waliohai wa aliyefariki.

 

Kawaida kijana wa kiume anarithi mara mbili kuliko msichana. Hii imewekwa na Muumba wetu kwa kuwa vijana wa kiume wana majukumu zaidi kishari’ah kuliko msichana. Hebu tutazame mfano ambao utakuwa rahisi kwa kila mmoja wetu kuufahamu. Mzazi amekufa ameacha kijana mwanamme na mwanamke na ameacha pesa taslim 300,000; kwa jinsi ya Mirathi mvulana atapata 200,000 na msichana 100,000. Laki moja ya msichana ni yake milki yake wala hapaswi kishari’ah kutumia chochote katika matumizi ya nyumba ila anapotaka mwenyewe kumsaidia kaka yake. Na kaka naye amepatiwa jukumu na shari’ah la kumtazama dada yake kwa makazi, chakula, matibabu na ikiwa anasoma basi atamlipia karo za shule.

 

Inapotokea kuwa mvulana anataka kuoa na msichana kuolewa, ni jukumu la mvulana kishari’ah kutoa mahari kwa anayetaka kumuoa na msichana kupokea mahari. Ikiwa mvulana atatoa mahari 100,000 na msichana kutaka 100,000 utakuta kuwa msichana yuko katika hali nzuri zaidi kuliko mvulana. Baada ya kuoa mvulana anawajibika kutazama nyumba yake, mkewe na watoto wake ikiwa atapata, ilhali msichana anatazamwa na mumewe kwa hali na mali isipokuwa anapotaka kufanya ihsani kwa kumsaidia mumewe.

 

Ukitazama haya utakuta kuwa wasichana wametunukiwa haki kubwa na nyingi na Muumba kuliko wavulana lakini hayo ni katika uadilifu wa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Na kinyume na unavyodhania kuwa wanaume wamependelewa.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share