06-Kwa Ajili Ya Allaah Kisha Historia: Ufupisho Wa Kushamiri Nadharia Ya Khumus

KAULI YA KWANZA: baada  ya  kukatika mfululizo wa  maimamu na kupotea kwa imamu mahdi ni kuwa khumus ni haki ya imamu asiye kuwepo,na wala  si ya fakihi wala mtukufu yoyote  na wala ya mujtahidina na kwa haya basi wengi wanadai zaidi ya watu ishirini kuwa wao ni  manaibu wa imamu aliyejificha kwa ajili ya  kuchukua khumus na wakasema: sisi tunakutana nae imamu aliye jificha, tunaweza  kumpa khums zote za vitega uchumi ambazo zina tujia.

Na lilikua hili katika nyakati za ghaiba ndogo (kujificha kudogo) na ikaendelea baada yake muda wa karne moja au mbili kipindi chote hicho haikutolewa khumus kupewa mujtahidin au mtukufu yoyote na katika  kipindi hiki vilionekana vitabu vine maarufu kwa jina la Assihahil-arbaai, na vyote hivi vimenakili kutoka kwa viongozi habari ya kuhalalisha khumus kupewa mashia na kuwaondolea mzigo wa kutowa ,,na hapa kuwepo na fatwa yeyote inayoruhusu kuwapa khumus  watukufu na mujtahidina.

 

 KAULI YA PILI: kisha likashamiri jambo la khumusi baada yakuwa mashia wameruhusiwa kutotowa khumsi wakati wa ghaiba , ikapatikana habari ya ulazima wa kutowa khumsi , ikiwa watu wenye mali wanataka kujiepusha na kauli ya kwanza , wakawa wanatakiwa kuitowa khumusi ili izikwe  mpaka atakapotoka Al-mahdi.

   KAULI YA TATU:  kisha likaendelea jambo la khumusi  wakasema ni wajibu kuiweka kwa mtu  muaminifu ,na walio bora kuchaguliwa kubeba amana hii ni wanazuoni wa madhehebu ya kishia, lakini inafaa kusisitiza kuwa uchaguzi huu ni bora tu na wala si lazima , na huyo mwanazuoni akipewa khumusi si ruhusa kuitumia bali kuiweka mpaka hapo atakapoifikisha kwa imamu Al-mahdi.

  Na hapa  kuna dokezo muhimu nalo ni kwamba ni nani kati ya wanazuoni wetu aliyehifadhi mali zilizoletwa kwake ,kisha baada ya kufa kwake wakasema warithi wake kuna mali zilizo wekwa amana kwa baba yetu ambazo sasa hivi zinapaswa kuwekwa kwa mtu anayechukuwa nafasi yake?

Bila shaka jawabu sahihi hapa ni kuwa :hakujapatikana mtu wa aina hii , wala hatujasikia wala kusoma habari za mtu kama huyu , ambae mali za watu (khumusi) zilikuwa kwake kisha baada ya kufa kwake zikahamia kwa aliye kuja baada yake.

 

 

   Na sahihi ni kwamba : kila aliyekewa amana ya mali wamekuja warithi wake nakugawana mali hiyo wakidai kua ni yao walirithi kutoka kwa baba zao ,kwahiyo khumusi ya imamu imekwenda kwa warithi wa mwanazuoni muaminifu , hali hii inajitokeza pale anapokuwa mwanazuoni huyo ni muaminifu na ile mali hakujifanya kuwa ni yake , je akiwa si muaminifu hali itakuaje?!!!

   Na inafaa kukumbuka zaidi kuwa  Qadhi ibn Bahraji au Baraji ndi aliyeliendeleza jambo la khumusi kutoka kwenye sunna na kufikia wajibu , kwa hiyo ndiye  aliyekuwa wa kwanza kusema ni dharura kuiweka shea ya imamu kwa anayeaminika miongoni mwa mafakihi na mujtahidina ili waikabidhi  kwa imamu aliejificha ikiwa watamkuta au ausiwe anaeaminika miongoni atakayekuja baada yake ili aikabidhi  kwa imamu. Na hili limeelezwa katika kitabu (AL-MUHADHAB  8/80) na hatua hii ni muhimu sana.

 

   KAULI YA  NNE: kisha wakaja maulamaa wa mwishoni mwishoni, wa kayaendeleza mas-ala ya khumsi kidogo kidogo mpaka iakafikia kusema kuwa niwajibu kutolewa khumsi  kupewa maulamaa  wazigawanye kwa wanao stahiki miongoni mwa mayatima na masikini wa ahlulu Bait,na habari yenye nguvu ni kuwa  fakihi bin Hamza ndie wa kwanza aliyevutika na kauli hii katika  karne ya sita kama alivyotoa ushahidi katika  kaitabu cha(Al-Wasilatu Fii Nayli Al – Fadhilat  uk:182) na akaliona hil;I la kuitowa khumsi kumpa mwanazuoni ni bora kuliko  kusimama mwenye khumus na kuigawa mwenyewe khasa ,ikiwa hajui kuigawa vizuri.

 

   KAULI YA TANO: yakaendelea mageuzi kidogo kidogo katika zama hizi na imekua kabla ya karne moja mpaka ukafikia uamuzi wa mwisho,baadhi ya  mafuqahi wakasema kuwa inaruhusiwa kutumia shea ya imamu katika baadhi ya mambo ambayo anayaona mwanazuoni kuwa ni muhimu kama kuwasaidia wanafunzi , na kusimamisha vituo vya dini, na mengeniyo kama alivyotoa fatwa Asayiud Muhsin Al Hakim katika Mustamsik( AL-Urwatu Al Uthqa 9/584).

 

 Kauli hii inaambatana na kauli ya kwamba hapana haja ya kurudi kwa mwanazuoni kutaka ushauri katika kuitumia sehemu ya imamu katika khumsi

 Na hii maana yake ni kuwa kule kutumia shea ya imamu katika khumusi  ni jambo lililojitokeza  katika zama hizi za mwishoni sana basi wao wanaiangalia hali yao ilivyo na kuona  mashule yao ,na vituo vyao uchapishaji na vitu vinavyo hitajika ni katika mambo yanayo faa kutolewa khumsi kwa ajili yake.

    Na vilevile wanaziangalia haja zao binafsi, basi vipi itawezekana  kukidhi haja zote hizi , hasa ukizingatia kuwa mambo yote haya yanahitaji pesa nyingi .

Ukawa mtazamo wao kwa khumusi njia nzuri ya kuwaingizia kiasi kitakacho kidhi haja zao zote na itakayowahakikishia manufaa yao binafsi na kuwapa utajiri kubwa sana kama tunavyoona leo hali ya wanazuoni ilivyo.

 Hakika kadhia ya khumsi imepitia duru nyingi na mabadiliko mengi mpaka mwisho ikatulia kuwa ni wajibu kuwapa khumus za vitega uchumi mafakihi  na mujtahidina (wanazuoni). Na kwa haya yanatubainishia sisi kua khumus haina hoja katika kitabu(Qur-ani) wala Sunnah wala kauli ya imamu bali hiyo ni kauli iliyodhihiri katika zama za mwishoni,wameisema baadhi ya mujtahidina, nayo ni yenye kupingana na Qur-an  na sunnah na viongozi wa ahlul Bait na maneno ya wanazuoni na fatwa za mafakih na mujtahidina na wenye kutegemewa.

    Nami na nawaomba  ndugu zangu na wanangu mashia wajizuie kutoa  khumus za vitega uchumi vyao na faida zao kwa watukufu wa mujtahidina,kwa sababu hiyo ni halali yao na wala si haki ya bwana mkubwa yoyote  au mwanazuoni yoyote,  Na wenye kutoa khumus kwa mwanazuoni au bwanamkubwa yoyote basi ajuwe ameingia katika madhambi kwa sababu ya kupingana na maneno ya maimamu kwa sababu khumsi si wajibu kwa mashia mpaka atakaporudi imamu mahdi .

 

    Na ninaona muhimu kautaja usemi wa Ayatulah Al Udhmaa Al Imamu A Khomeiniyu katika mas-ala haya, kwani alizungumza kuhusu khumusi katika mihadhara aliyoitowa tukimsikia sote katika chuo cha cha  Najaf mwaka [1389 H]Kisha akakusanya katika kitabu Al-Hukumatul Al Islamiya au  Walayatul Al Faqih:  miongoni mwa aliyokuwa ameyasema: tutakuwa tuna uoni mfupi tukisema kwamba khumusi imeletwa kwa ajili kulinda maisha ya watoto wa mtume (s.a.w) peke yao.

 

Akendelea kusema kuwa inawatosha wao na kubaki sehemu ndogo tu ya maelfu ya mali yote ya khumusi  bali wanatoshwa na khumsi ya soko moja tu kama vile soko la Iraki kwa mfano miongoni mwa masoko mengi makubwa kama vile masoko ya Irani Sirya na Islama bad na mfano wa hayo , sasa mali inayo baki itakuwaje?

   Kisha akasema : hakika mimi ninaona hukumu ya kiislamu ya uadilifu, haitaki  kufanyiwa takhlifi  kubwa katika mambo ya upuuzi au kinyume na maslahi ya wote.

 Kisha anasema:  haikuwa kodi ya khumus ni kwa ajili ya kudhamini maisha ya mabwana wakubwa katika familia ya mtume (s.a.w) tu wala zaka si kwa ajili kwatenganisha mafakiri na masikini isipokuwa khumsi na zaka zinakuwa zaidi ya hajja za hao waliotajwa ,

    Basi je baada ya hayo uislamu  utaacha kuzuia  kitendo hicho cha khumus na zaka na  yanayo fanana na mtazamo wa kuizibia haja watukufu na masikini au itakuwa marejeo yao zaidi chakula cha bahari au kuzikwa chini au mfano wake?.

   Walikuwa watukufu wengi miongoni mwa wanao ruhusu kupata  ruzuku katika khumus siku hizo,yaani mwanzo mwanzoni mwa uislamu, hawavuki mia moja  na lau tungekisia idadi yao kuwa ni nusu milioni,je ingekuwa inaingia akilini kuwa uislamu unajishughulisha kwa kufaradhisha khumsi ambayo ni mali nyingi sana na zinazidi siku hadi siku yote hayo kwa ajili ya kushibisha familia ya mtume (s.a.w).

  Yote hayo  angalia kitabu chake kilichotajwa,[1/39-40-42] chapa ya Al Adab Annajaf.

 Hakika imamu Al Khomeniyu  anaweka wazi kuwa mali ya  khumus ni nyingi sana,hii ilikua wakati huo pindi alipo kuwa ni muhadhiri wa chuo cha najaf basi je  ni wingi wa mali ulioje ukizingatia katika zama zetu hizi?.

   Na imamau pia  ameweka wazi kua sehemu moja katika maelfu ya sehemu ya mali hii kubwa inatosha kwa Ahlul, Bait wa Mtume(a.s.w)  na  ahli zake, basi je wataifanyeje sehemu kubwa ya mali  iliyo bakia?.  Imamu khomeni ana maana kwamba ni lazima kuzigawa mali hizi zinazo baki kwa mafakih na mujtahidina (wanazuoni) kutokana na  ufahamu wa usemi wa imamu Al Khomeniy.

    Kwa sababu hii imamu khomeni alikua na utajiri mkubwa sana alivyokuwa akiishi Iraqi na alipotaka kusafiri kwenda ufaransa kwa kuishi huko alizigeuza pesa zake kutoka dinari za Iraqi kuziweka kwenye dola za kimarekani na akazihifadhi katika mabenki ya ufaransa na kupata riba kubwa sana.

 Hakika uharibifu wa mtu unakuja kwa njia mbili :- kwa njia ya kijinsia na mali na vyote hivyo vinapatikana kwa watukufu, upande wa kijinsia wanaupata kwa njia ya mut’a na isiyokuwa mut’a , mali wanazipata kwa njia ya khumusi na zile zinazotupwa makaburini , ni nani kati yao atakayeweza kupambana na vishawishi hivi , ukizingatia wengi wao wameifuata njia hii kwa ajili ya kushibisha matamanio yao ya ngono na mali ?!!

 

Share