Kajuana Na Kijana Katika Mtandao (Internet) Ambaye Anataka Kumposa Lakini Anataka Kujua Yukoje Kimaumbile

SWALI:


Asalamu alaikum warahmatullahi wabarakatu. Bismillahi rahmani rahim
Ndugu waislamu, nina swali hii ambayo inanitatiza sana nilijuwana na kijana katika internet, kijana mwenye heshima na adabu, mimi Alhamdullilah ni msichana nimeshika swala zangu tano Alhamdullilah. Sasa mimi nazungumza na huyu kijana katika email yangu nataka mujuwe kuwa siku moja hatukuzungumuza kitu kinacho udhi. hadithi zote ni ya adabu na kuhusu dini...Sasa huyu kijana amependezwa na tabia yangu na anataka kuja kwa wazee wangu kuni posa, lakini ameniambia nimweleze mimi niko vipi kuwa sisi bado hatujaonana yaani kama ni mrefu, mfupi, mwembamba au mnene. Sasa swali yangu ni hili ni sawa nikimweleza ama si sawa. Nasubiri jibu >>>........ Waalaikum salam warahmatullahi wabarakatu..............

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukran kwa swali lako kuhusu kijana kutaka kujua sifa zako za kimaumbile kwa ajili ya kuja kukuposa.

Katika shari’ah ya Kiislamu, inazuilia jambo lolote ambalo linamkaribisha mtu katika uzinzi/ zinaa na linakaribisha ndoa pamoja na vikwazo vyake vya kutokwenda katika zinaa.

 

Ikiwa hilo tu ndilo alitakalo waweza na ni ruhusa kumueleza kuwa wewe kwa mfano ni mwembamba, mrefu na maji ya kunde. Hiyo inatosha kabisa wala usitume picha yako kwa hali yoyote ile. Ikiwa ameridhika na wasifu wako wa jumla anaweza kufunga safari kuja kukuona wewe nyumbani kwenu ukiwa na wazazi wake la si hivyo uhusiano huo utakuwa haufai.

 

Inatakiwa tutahadhari sana na marafiki wa kwenye mtandao (internet), kwani wengine hujionesha kuwa ni wazuri kisha kutumia fursa ya kuaminiwa kufanya maovu.

 

Kadhalika ni vizuri binti wa Kiislamu kujichunga na mahusiano na wanaume kwenye mtandao bila idhini au ufahamu wa wazazi wake au kaka zake. Na hivyo hivyo mwanamme ajiepushe na mawasiliano na wanawake kwenye mtandao. Mara nyingi hupelekea mahusiano yasiyo ya kishari’ah.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share