Du’aa ya Kuwaombea Watoto Ili Wawe Wanaswali Daima

SWALI:

 

Asalam alaikum warhmatullahi wabarakat naomba dua lolote zuri sana na mjarab niombee wanangu wasali bila ya kuhimizwa.


 

JIBU: 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. 

Shukrani kwa swali lako kuhusu du’aa ya kuwaombea watoto wawe ni wenye kuswali.

Hakika mwanzo kabla ya kuwaombea du’aa inatakiwa uwape watoto wako malezi mazuri, nawe pia uwe mfano mwema kwa kuswali pamoja nao, kuwapeleka Madrasah kufundishwa Diyn na kuwasuhubisha na watoto wenye marika yao walio wema. 

Baada ya hapo muombe Allaah Aliyetukuka kwa du’aa yoyote ile inayolingana na matakwa yako. Na miongoni mwa du’aa nzuri ni ile aliyoomba Nabii Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) inayoesema: “Rabbij’alniy Muqiymasw Swalaati wa min Dhurriyyatiy Rabbaana wa Taqabbal Du’aa’ - Mola wangu Mlezi! Nijaalie niwe mwenye kusimamisha Swaalah, na katika dhuriya zangu pia. Ee Mola wetu, na ipokee du’aa yangu” (Ibraahiym [14]: 40).

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share