Wanaume Kuvaa Tai Inafaa?

 

Wanaume Kuvaa Tai Inafaa?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Assalaam Aleyikum

 

Mimi napenda kupata ufafanuzi kuhusu vazi la tai kwa sisi waislam je linafaa kuvaliwa au ni makosa kulivaa na kama linafaa je huu si utamaduni wa mayahudi ambao sisi waislam haufai kuiga? Kwani tunaambiwa yoyote anayejifananisha na mayahudi na makafiri basi ni miongoni mwao. Na kama halifai ni mavazi gani mengine ambayo sisi waislam hatupaswi kuyavaa.

 

Wabillah Tawfiq

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Msingi ambao Uislamu umeweka katika mavazi ni kuwa ni halali kuvaa, isipokuwa yale yaliyokatazwa na sheria, kama dhahabu na hariri kwa wanaume.

 

 

Wanachuoni mbalimbali wametofautiana na vazi la tai; kuna walioona kuwa ni vazi la kikafiri na pia linawakilisha msalaba na hivyo halifai kuvaliwa, nao ni kama Shaykh Al-Albaaniy na wengine, Na wengine wamesema tai si vazi makhsusi kwa makafiri wala Wakristo kama Shaykh ‘Abdul-‘Aziyz bin ‘Abdillaah bin Baaz na wengineo.

 

 

Hivyo, vazi hilo lina utata pamoja na kuwa kuna wanaosema kuwa haliwakilisha msalaba na si vazi makhsusi kwa makafiri, lakini hatuoni faida yake wala umuhimu wake kuivaa kwani haistiri uchi wala haikingi baridi wala kuihifadhi mwili na chochote zaidi ya kuwa ni pambo tu tena lenye mwelekeo wa kifakhari. Hivyo, ni bora Muislam kujiepusha na mavazi ya aina hiyo.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share