Adhkaar Katika Rukuu Na Sujuud

SWALI:

 

Assalaam alaykum alaykum alhidaaya, kwanza samahani kwa kuuliza maswali kwani siruhusiki kwa majibu ya maelezo lkn sheikh nakuomba unitowe wasiwasi kama utapata muda ili nijuwe vipi ibada yangu naitekeleza sahihi ama na hasa mwezi huu mtukufu isije ikawa nafanya ibada kumbe nakwenda kinyume. 

 

Moja, ni kuhusu adhkar za rukuu na sujudu nimeona ktk hiswnul muslim wameandika kwa namba, je mie natakiwa nizisome zote kama za sujudu au nichague moja halikadhalika na rukuu.


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu Adhkaar za rukuu na sujuud.

Hakika mwandishi wa Hiswnul Muslim, Allaah Aliyetukuka Amjaze kheri amejaribu kukusanya Hadiyth zote au nyingi zinazohusiana na Adhkaar alizokuwa akizileta Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa katika rukuu au sujuud.

Nazo zinapatikana katika viungo vifuatavyo:

 

 

Inavyotakiwa ni kuchagua Adhkaar moja ambayo utaisoma katika rukuu na nyengine katika sujuud kati ya hizo zilizoandikwa. Hata hivyo, ikiwa unaswali peke yako na unarefusha rukuu au sujuud kama alivyokuwa akifanya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) basi unaweza kuchanganya Adhkaar kadhaa ili rukuu na sujuud ziwe ndefu.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share