Maduka Kutoa Mkopo Na Kupanga Muda Wa Kulipa Kwa Kiwango Fulani Ziada Je Ni Ribaa?

SWALI:

 

Asalam alaykum warhamatulahi taala wabarakatu. Napenda kuuliza kuna maduka mengine huku ulaya wanakopesha vitu na wanakupangia mda wa kulipa na wanakupangia kiasi cha kulipa. Lakini wanaweka pesa kida ziada na ukiwauliza kama hi ni riba wanasema sio riba ni pesa ya ushuru wa kulipia karasi ya kalipia deni, kwa hiyo wanatoza dola 4 ziada kila mwezi, je hii siyo riba.

 


 

 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu maduka Bara Ulaya yanayo kopesha vitu na kulipa ziada.

 

Ikiwa tumelifahamu vyema swali lako hilo ndugu yetu ni kuwa wewe unanunua bidhaa ambayo huna pesa taslimu, sasa mwenye duka anakusaidia kwa kukuruhusu kulipa polepole kwa muda fulani. Ikiwa ni hivyo maduka kama hayo yapo hata Afrika Mashariki na huo mkopo wa kulipa polepole unaitwa Hire Purchase (lipa polepole), au ‘buy now pay later’. Ikiwa ni hivyo, biashara hiyo na nyongeza au mkopo wa aina hiyo unaruhusiwa na si riba. Itakuwa haifai tu pindi itakupokuwepo sharti la kuwa usipoweza kulipa kwa kipindi fulani, basi utalipa na ziada (riba). Hapo itakuwa haifai kabisa.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share