Masiyh Ad-Dajjaal Atafufuliwa Tena Siku Ya Qiyaamah Kufitinisha Watu

SWALI:

 

Assalaam Alaykum Warahmatul Laahi Wabarakat Ama Baad, Mashehe zetu tunakutakieni kila la kheri na kazi zenu za daawa na inshaala Allaa Mwenyezi Mungu akujaalieni pamoja na sote, ama nimesoma kwa urefu makala yenu kuhusu massihi dajaali kwa namna atakavotokea na mpaka kuuliwa kwake. sasa mimi nauliza suala huyu dajaali baada ya kufa atafufuliwa tena siku ya kiaama na kuanza kufitinisha kama alivofanya hapa duniani, ni hayo tu ila majibu yetu mnatuchewesha lakini Inshaalla Allaah atakufanyieni wepesi.

 

Maasalaam,

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu Masiyh ad-Dajjaal na kufufuliwa kwake.

Masiyh ad-Dajjaal ni kiumbe ambaye Ataletwa na Allaah Aliyetukuka kabla ya Qiyaamah na atafishwa kabla ya Siku ya Qiyaamah.

 

Hakika ni kuwa viumbe vyote ambavyo vitaishi hapa duniani wanaadamu au majini wamekalifishwa kufuata yaliyo mazuri na kuacha yaliyo mabaya. Mwenye kufuata atapata ufanisi wa duniani na Kesho Akhera na wenye kukengeuka basi watapata adhabu hapa duniani na kubwa zaidi Siku ya Qiyaamah. Kwa hiyo, bila shaka Masiyh atafufuliwa na kuhukumiwa na Allaah Aliyetukuka.

 

Tafadhali sikiliza mawaidha haya hapa chini upate faida zaidi.

 

Masiyh Ad-Dajaal

Masihi Dajjaal Wazazi Wake

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share