Kuna Uharamu Kufanya Biashara Na Benki Na Kama Upo Ni Nini Uharamu Wake?

SWALI:

 

ASSALAM alykum wa -RAHMA tuh wa barakatuh. MWENYEZI MUNGU akujaliyeni kila la kheri na afya njema. Nina shukuru kwa msaada wenu na kwakujitolea kutu elimisha.

 

Swaali langu nikuomba kuelimishwa mimi na wenzangu kuhusu maisha tunao kwa wakazi wa europa. Je, ni haramu kufanya biyashara na benki, nini uharamu wake?

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu uharamu wa kufanya kazi benki.

Kufanya kazi benki ni haramu kwa Muislamu mwenye kuipenda Dini yake hii ya Uislamu. Uharamu wake ni kuwa benki hizo zinatumia mfumo wa ribaa ambao umeharamishwa na Allaah Aliyetukuka pamoja na Mtume wake (Swalla Allaahu ‘alayhi  wa aalihi wa sallam).

 

Hakika Allaah Aliyetukuka Amekuwa mkali sana kuhusu ribaa kiasi ambacho kamwelezea mtu mwenye kutekeleza hilo ametangaza vita Naye. Anasema Aliyetukuka:

Enyi mlioamini! Mcheni Allaah, na acheni ribaa zilizobakia, ikiwa nyinyi ni Waumini. Basi mkitofanya jitangazieni vita na Allaah na Mtume Wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilmali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe” (al-Baqarah 2: 278-279).

Je, tunaweza vita na Allaah Aliyetukuka?

Na tufahamu kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi  wa aalihi wa sallam) amekataza (ameharamisha) kuchukua na kutoa ribaa (al-Bukhaariy).

 

Na miongoni mwa madhambi saba yenye kuharibu ‘amali za mja, mojawapo ni kula ribaa (al-Bukhaariy).

 

Na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi  wa aalihi wa sallam) amemlaani mwenye kutoa na kupokea ribaa (al-Bukhaariy).

 

Benki hizi za kawaida msingi wake mkubwa ni ribaa hivyo kufanya ufanyaji kazi wa sehemu hiyo kuwa haramu.

 

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo na manufaa zaidi:

 

 

 

Jinsi Benki Za Kiislamu Zinavyotoa Huduma Zake

 

 

Anayefanya Kazi Benki Anahesabiwa Kuwa Ni Mpokea Rushwa? Nini Hukumu Ya Kufanya Kazi Banki?

 

 

Kufanya Kazi Katika Shirika La Riba

 

Kazi Katika Uislam

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share