Kurejesha Mkopo Wa Benki Bila Kulipa Ribaa

SWALI:

NI AINA GANI ZA BIASHARA NI HARAM?

KUNA BAADHI YA BENKI WANAPOTOA MIKOPO MNAKUBALIANA KUREJESHA KWA RIBA LAKINA UKIPATA HASARA AMBAYO KWENYE "BUSSINES PLAN" YAKO NI KOSA LA KITAALAM HAWACHUKUI DHAMANA ULIOWEKA JE MSINGI HUU KWA ALLAH UKOJE? YANI KUTOREJESHA ULICHOPEWA UKIACHILIA MBALI RIBA AMBAYO HUJAPATA.

ARSHUDUUNY YAR HAMKUMULLAH                                                    


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu kurudisha mkopo wa benki bila ya ribaa. Mwanzo mwenye kukubali kuchukua mkopo ambao ataulipia ribaa amefanya dhambi kubwa. Inabidi Muislamu atubie sana kuhusiana na kosa hilo alilolifanya.

Bila ya shaka yoyote ile benki za kawaida ambazo zinategemea ribaa huwa hazichukulii kabisa mas-ala dhamana kwa hasara yoyote ambayo mkopesha atapata. Wao lao ni kupata kutoka kwako mlichoahidiana bila kutazama umepata hasara gani au faida ngapi. Mkataba wowote ambao unafanywa kwa kuingizwa haramu unakuwa hauwezi kuchukuliwa na wala haufai kabisa kutimizwa.

Hata hivyo, tunaishi katika dola ambazo si za Kiislamu na mkataba kama huo unachukuliwa ni halali na ni lazima mkopeshwa arudishe pamoja na ribaa hiyo. Kutorudisha kutakuingiza matatizoni na kuweza ima kupigishwa mnada vitu vyako ili kulipa gharama hizo au kuingizwa jela kwa kutolipa deni la wenyewe.

Kwa hali hiyo, itabidi ufanye bidii ulipe na usiingie tena katika mikataba haramu yenye laana na uombe msamaha kwa Mola wako.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share