Deni La Swawm Inafaa Mtu Mwingine Kumlipia? Swawm Infaa Katika Hedhi?
SWALI:
assalaam alaykum warahmatullah wabarakatu.mwenyeezi mungu mtukufu akujaarieni kheri kwa kutuelimisha.swali langu ni hivi;mimi siumwi,ninadeni la faradhi ya ramadhani.je mama yangu anaweza kunisaidia kufunga?tunafunga sote tukimaanishsa siku moja kwa malipo ya siku mbili.nilifungua wakti wa hedhi.je inaswihi?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Haifai mtu yeyote kumlipia mwingine deni la Swawm, kwani Fardhi hii ya Swawm inampasa kila Muislamu aliyekuwa baleghe, mwenye akili timamu, asiye na udhuru wa ugonjwa wa kumzuia kufunga Ramadhaan. Haifai kufanya hivyo hata
((وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَى وَإِن تَدْعُ مُثْقَلَةٌ إِلَى حِمْلِهَا لَا يُحْمَلْ مِنْهُ شَيْءٌ وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَى))
((Wala hatabeba mbebaji mzigo wa mwingine. (Kila mtu atachukua jukumu ya dhambi zake mwenyewe). Na
Vile vile kila mtu atachuma yale tu aliyoyafanya yeye na atalipwa kwa mema au maovu aliyoyafanya:
((أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَى)) ((وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلَّا مَا سَعَى)) ((وَأَنَّ سَعْيَهُ سَوْفَ يُرَى)) (( ثُمَّ يُجْزَاهُ الْجَزَاء الْأَوْفَى))
((Ya kwamba haichukui nafsi dhambi za nafsi nyingine))
((Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyoyafanya mwenyewe))
((Na kwamba vitendo vyake vitaonekana))
((Kisha ndio atalipwa malipo yake kwa ukamilifu))
[An-Najm:38-41]
Kwa hiyo
Kuhusu kufunga katika hedhi, pia haifai Swawm yako itabidi pia uzilipe hizo siku ulizofunga katika hedhi. Mwanamke katika hedhi hatakiwi kufunga Swawm wala kusali, lakini anatakiwa alipe deni
Na Allah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


