Maana Ya Swawm Na Historia Yake
Maana Ya Funga
Maana ya kufunga (Swawm) ni kujizuilia. Neno Swawm kwa maana ya kujizuilia linaweza kutumika katika kujizuia kufanya jambo lolote la kawaida mtu alilozoea kulifanya. Katika Qur-aan tunafahamishwa kuwa Bibi Maryam baada ya kumzaa Nabii ‘Iysaa (‘Alayhis Salaam) alijizuia (alifunga) ili asiseme na mtu neno lolote juu ya mtoto wake.
“...Na
Katika Uislamu kufunga (Swawm) ni kujizuilia kula, kunywa, kuvuta sigara, kuingiza kitu chochote katika matundu mengine mawili kama vile pua na masikio, kujizuia na kujamii, kujitoa manii kwa makusudi au kwa matamanio na kujizuia kujitapisha kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), kwa kipindi cha kati ya Al-fajri ya kweli mpaka kuingia magharibi. Hii ndio maana ya nje ya Swawm katika Uislamu.
Kufunga katika Uislamu kuna maana ya ndani zaidi, ambayo
Kufunga kwa maana ya ndani ni pamoja kujizuilia kutenda maovu yote yaliyokatazwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Ili Swawm ya mfungaji iwe na maana na yenye kufikia lengo, hana budi kukizuilia (kukifungisha) kila kiungo chake cha mwili - macho, ulimi, masikio, mikono na miguu- pamoja na fikra na hisia zake na matendo aliyokataza Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala).
Funga ya macho ni kujizuilia na kuangalia aliyoyakataza Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala); Funga ya ulimi ni kujizuilia na mazungumzo yote aliyoyakataza Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kama vile kusengenya, kusema uwongo, kugombana na kadhalika, funga ya masikio ni kujizuia kufanya yale yote aliyoyaharamisha Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala); funga ya miguu ni kujizuilia na kuendea yale yote aliyoyakataza Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) funga ya fikra na hisia ni kujizuia na fikra na dhana mbaya ambazo zinampelekea kuvunja amri na makatazo ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Ni katika maana hii Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)anasema katika Hadithi zifuatazo:
Abu Hurayrah amesimulia kuwa Mtume wa Allaah amesema:
“Yule ambaye haachi kusema uwongo na haachi kufanya vitendo viovu, Allaah hana haja na kuona kuwa anaacha chakula chake na kinywaji chake (yaani Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) hana haja na funga yake.” (Al-Bukhaariy).
Abu Hurayrah ameeleza kuwa Mtume wa Allaah amesema:
“Ni wangapi wanaofunga lakini hawana funga ila kukaa na kiu tu ni wangapi wanao swali usiku ambao hawana Swalah ila huambulia kupoteza usingizi tu.” (Ad-Daarimiy).
Hadithi hizi zinatuthibitishia kuwa ufungaji usioambatana na kujizuia na mambo maovu na machafu, haumpatii mfungaji faida yoyote.
Funga ya Ramadhaan ni miongoni mwa nguzo za Uislamu na ni faradhi kwa Waislamu kama inavyobainika katika aya ifuatayo:
“Enyi mlioamini! Mmeamrishwa kufunga (Swawm)
“Kuna viungo vitatu vinavyomuunganisha Muislamu na dini ya Uislamu na yeyote yule atakayevunja kiungo kimoja katika hivi atakuwa amekana Uislamu na kuuawa kwani ni halali. Viungo hivi ni: Kushuhudia kuwa hapana Mola ila Allaah, Kusimamisha Swalah tano na kufunga mwezi wa Ramadhaan.”
Katika Hadiyth nyingine Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
“Yeyote yule atakaye acha makusudi kufunga siku moja ya mwezi wa Ramadhaan, hawezi kuifidia siku hiyo hata akifunga kila siku katika umri wake wote (uliobakia).” (Abu Daawuud)
Funga ni ibada maalum iliyo muhimu
Abu Hurayrah ameeleza kuwa Mtume wa Allaah amesema:
“Mwenye kufunga Ramadhaan akiwa na imani na akawa na matumaini ya kupata malipo kutoka kwa Allaah dhambi zake zote zilizopita husamehewa, Na mwenye kusimama kwa Swalah (tarawehe) katika mwezi wa Ramadhaan akiwa na imani na matumaini ya kupata malipo (kutoka kwa Allaah), dhambi zake zote zilizopita zitasamehewa. Na yule atakayesimama (kwa Swalah) katika usiku uliobarikiwa (Lailatul-Qadri) akiwa na imani na matumaini ya kupata malipo kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) dhambi zake zote zilizotangulia zitasamehewa.” (Al-Bukhaariy na Muslim).
Pia Abu Hurayrah ameeleza kuwa Mtume wa Allaah amesema:
“Kila amali njema anayoifanya mwanaadamu italipwa mara kumi (Al-Qur-aan 6:160) mpaka kufikia mara mia saba (Al-Qur-aan 2:261). Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) amesema:
Historia Ya Kufunga
Funga, kama ilivyo katika ibada nyingine
Enyi mlioamini! Mmeandikiwa (mmefaradhishiwa) kufunga
Katika historia tunajifunza kuwa, kila Mtume alipoondoka, baada ya kipindi kupita, watu waliacha mafundisho yake na kuingia katika ushirikina. Lakini bado tunakuta funga, japo si katika madhumuni na asili yake iliyoachwa na Mitume wa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), imebakia katika jamii za kishirikina kwa kipindi chote cha historia. Hebu tuangalie mifano michache ya dini za ushirikina ambapo funga, kwa maana ya kushinda na njaa na kiu, imekuwa miongoni mwa ibada muhimu za dini hizo.
Jamii Ya Nabii Ibraahiym
Nabii Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) aliinuliwa katika jamii ya washirikina. Walikuwa wakiabudu jua, mwezi, nyota na masanamu chungu nzima waliyoyachonga wenyewe. Pamoja na ushirikina wao huo walikuwa wakifunga siku 30 mfululizo katika kila mwaka kwa heshima ya mwezi.
Wahindu (Hinduism)
Dini ya Kihindu ni miongoni mwa dini za kishirikina katika bara la
Mayahudi (Judaism)
Dini ya Kiyahudi ni dini waliyoibuni Mayahudi baada ya Nabii Muusa (‘Alayhis Salaam) ambapo walimfanya Uzairi mwana wa Mungu. Pamoja na hivyo wachaji wa Kiyahudi walikuwa wakifunga Alhamisi na Jumatatu
Pia Mayahudi hufunga kwa saa 24 katika kila mwezi 10 Muharamu, kwa kumbukumbu ya siku Wanaisraili (Mayahudi) walipookolewa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kutokana na udhalimu wa Fir’awn. Siku hii ambayo hata Waislamu wamesuniwa kufunga huitwa siku ya ‘Ashuuraa.
Pamoja na funga hizi, pia Mayahudi wana tabia ya kufunga mara kwa mara kulingana na haja. Kwa mfano mtu anaweza kuamua kufunga siku kadhaa kama kumbukumbu ya matukio fulani katika maisha yake, au anaweza kufunga funga
Ukiacha siku ya ‘Ashuuraa ambapo funga huchukua saa 24, funga za Mayahudi huanza alfajiri na huishia pale inapojitokeza nyota ya kwanza usiku.
Wakristo
Dini ya Ukristo imebuniwa baada ya Nabii ‘Iysaa (‘Alayhis Salaam). Katika dini hii Nabii ‘Iysaa (‘Alayhis Salaam) amefanywa mwana wa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na kwamba yeye ndiye mkombozi wa Wakristo. Pamoja na hivyo, Wakristo wanakiri kuwa kufunga ni kitendo cha uchaji - katika dini
Historia inatuonyesha vile vile kuwa funga hizi za Washirikina zimetofautiana
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
