Ramadhaan-Swawm

Ramadhaan-Swawm

Kubakia Imara (Thabiti) Baada ya Ramadhaan

Kubakia Imara (Thabiti) Baada ya Ramadhwaan

 

Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Share

Nini Baada Ya Ramadhwaan?

Tumeuaga mwezi wa Ramadhwaan, mwezi wenye Baraka na Rahmah. Tumeaga mchana wake tulipokuwa katika subira ya Swawm, na usiku wake tulipoonja ladha ya Qiyaamul-Layl (kusimama usiku kuswali). Tumeuaga mwezi wa Qur-aan, mwezi wa taqwa, mwezi wa jihaad, mwezi wa maghfirah, mwezi wa kuomba du'aa kwa wingi, mwezi wa kuepushwa na Moto. Amefaulu aliyetimiza Swiyaam ilivyopaswa akachuma thawabu nyingi na akajitahidi kuzidisha ‘ibaadah. Lakini amekula hasara aliyepuuza Swiyaam na hukmu zake na kutokujitahidi katika ‘ibaadah.    

 

Kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) katika Aayah zilizofaridhishwa kufunga Swiyaam katika Ramadhwaan kuwa lengo la Swiyaam ni taqwa.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٨٣﴾

Enyi mlioamini! Mmeandikiwa Swiyaam kama ilivyoandikwa kwa wale ambao wa kabla yenu mpate kuwa na taqwa [Al-Baqarah: 183]

 

Kila Muislamu aliyeingia katika mwezi wa Ramadhwaan atakuwa ameingia na ametoka katika madrasa ya taqwa. Na mtu anapoingia katika madrasa yoyote ile, hutoka humo akiwa amepata manufaa au shahada ya lile somo alilolisoma, na baada ya hapo...

 

Share

Pages

Subscribe to RSS - Ramadhaan-Swawm