Ma’muul Za Lozi (Lebanon)

Ma’muul Za  Lozi (Lebanon)

 

 

 

Vipimo:

 

Siagi   -  400 gms

Sukari -  2 vijiko vya supu

Unga - 4 – 5 vikombe

Mayai  -    2

Vanilla   ½ kijiko cha chai

Lozi  - 2 vikombe

Sukari ya unga (icing sugar) - 1 kikombe

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika.

 

  1. Tia siagi na sukari katika mashine ya keki kisha usage hadi iwe laini kabisa.
  2. Tia ute wa mayai uchanganye vizuri.
  3. Tia vanilla
  4. Tia lozi zilomenywa na kukatwakatwa slaisi (blanched sliced almonds).
  5. Tia unga kidogo kwanza katika mashine uchanganye vizuri. Kisha zima mashine na uendelee kutia unga kidogo kidogo ukichanganya kwa mkono hadi ushikane.
  6. Tia katika mbao ya ma’muul (kama kwenye picha) ubonyeze ndani ili itengenezeke duara.

 

   

 

  1. Vipange katika treya ya kupikia katika oveni.
  2. Choma (bake) kwa moto mdogo kabisa takriban 300°C .
  3.  Vikiiva vitoe viache vipoe kisha nyunyizia sukari ya unga (icing sugar) na uviweke katika vijikombe vya karatasi.

Kidokezo:

 

Kiasi cha unga hadi mchanganyiko wa Ma’muul ushikane inategemea saizi ya mayai. 

 

Share