Kuoa Dada Wawili Kwa Pamoja

SWALI

Assalam alaikum.

 naomba mniweke wazi katika sheria hivi ndugu halisi wa bibi yangu mfano bibi yangu anaitwa raya  issa ndugu yake anaitwa salma issa jee itajuzu yaani inafaa kumuowa huyu ndugu yake yaani salma issa ahsante?

 


JIBU: 

Shukrani kwa swali lako na natumaini tutafaidika sote katika kulijibu swali hilo.

Sifa zote njema Anastahiki Allah Mtukufu, Swalah na salamu zimfikie kipenzi chetu, Mtume Muhammad (s.a.w.w.), Ahli zake na Maswahaba wake (r.a.) na Watangu Wema na waliowafuata kwa kheri mpaka Siku ya Kiyama. 

Uislamu ni Dini ambayo ina sheria iliyo sambamba na maumbile ya mwanadamu na hakuna jambo lolote isipokuwa Allah Ametuelezea. Allah Anasema:

Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote ().

Hivyo, katika mas-ala ya ndoa Allah Ametuwekea wazi wale ambao unaweza kuwaoa na wale ambao huwezi kuwaoa. Na katika usiyeweza kumuoa ni dada ya bibi yako (mkeo).

Allah Anasema:

"Mmeharimishiwa mama zenu, na binti zenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na khaalati zenu, na binti wa ndugu mume, na binti wa dada, na mama zenu waliokunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu waliozaliwa na wake zenu mliowaingilia. Ikiwa hamkuwaingilia basi hapana lawama juu yenu. (Pia mmeharimishwa) wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu. Na kuwaoa pamoja dada wawili isipokuwa yale yaliyokwisha pita. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu"

 (). 

Kwa ajili hiyo huwezi kisheria kumuoa Raya binti Isa na dada yake Salmah binti Isa, lakini ikiwa Raya ataaga dunia au utamuacha unaweza kumuoa dada yake wakati huo.

Na Allah Anajua zaidi.

 

Share