Visheti Vya Kastadi Vya Shepu Ya Kombe

Visheti Vya Kastadi Vya Shepu Ya Kombe

 

   

 

Vipimo

 

Unga wa ngano  -   1 Kilo

Siagi -  ¼ kilo

Mayai    2

Kastadi  (custard)  -  3 vijiko vya supu

Baking powder -   1 kijiko cha chai

Maziwa  -    1 ½ gilasi

Mafuta Ya kukaangia -   kiasi katika karai

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Weka unga katika bakuli kubwa kisha changanya na unga wa kastadi na baking powder.
  2. Tia siagi uchanganye vizuri.
  3. Tia mayai, kisha maziwa ya baridi uchanganye vizuri usiukande sana.
  4. Fanya madonge kisha kata vipande vidogovidogo kisha ubonyeze kwa kidole uvikwaruze kwenye chujio lenye tundu itokee shepu (design) yake. 

         

 

5-  Tia mafuta katika karai yakipata moto, kaanga visheti hadi viive. Usiache hadi vikageuka rangi sana.

6-  Eupua, weka katika sufuria au chombo kikubwa kusubiri shira.

 

Vipimo Vya Shira

Sukari -  ½ kilo

Hiliki  ilosagwa  -  1 kijiko cha chai

‘arki (rose flavor)  -   5 matone

Maji -  1 gilasi

 

Namna Ya Kutyarisha

  1. Changanya sukari na maji uipike hadi iwe nzito.
  2. Ukiona mapovu yanatoka tia hilik na ‘arki .
  3. Mwagia katika visheti uchanganye vizuri hadi vishike na sukari.                                                                           

 

 

 

Share