Pilau Ya Nyama Kusaga, Adesi Za Brauni Na Zabibu (UAE)

Pilau Ya Nyama Kusaga, Adesi Za Brauni Na Zabibu (UAE)

 

 

Vipimo

Mchele wa Par boiled au basmati - 5 vikombe

Nyama kondoo/mbuzi ya kusaga - 1 kikombe

Kitunguu - 2

Kitunguu saumu (thomu/galic) - 7 chembe

Adesi za brauni (brown lentils) - 1 kikombe

Zabibu - 1 kikombe

Baharaat/bizari mchanganyiko - 1 kijiko cha supu

Chumvi - kiasi

Pilipilii manga - ½ kijiko

Jiyra/bizari pilau/cummin - 1 kijiko cha chai

Supu ya nyama ng’ombe - Kiasi cha kufunikia mchele

Mafuta - ½  kikombe

 

Namna Ya Kutayarisha

Osha, roweka masaa 2 au zaidi.

Katakata (chopped)

Menya, saga, chuna

Osha, roweka, kisha chemsha ziive nusu kiini.

Osha, chuja maji

 

Namna Ya Kupika:

  1. Tia mafuta katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vianze kugeuka vyekundu.
  2. Tia kitunguu thomu, kaanga, tia baharati/bizari zote kaanga.
  3. Tia nyama uchanganye vizuri, ukaange iwive..
  4. Tia mchele ukaange kidogo kisha tia supu, koroga kidogo, funika uivie mchele.
  5. Karibu na kuiva, tia adesi, zabibu, changanya, funika uendelee kuiva kama unavyopika pilau.
  6. Epua pakua katika chombo, ongezea zabibu kupambia ukipenda.

 

Adesi Za Brauni:

 

 

 

 

 

 

 

  

 

Share