Mbatata/Viazi Vya Nazi Kwa Nyama Ya Ng'ombe

Mbatata/Viazi Vya Nazi Kwa Nyama Ya Ng'ombe

  

 

Vipimo

Mbatata / viazi - 2 kilo

Nyama ng’ombe - ½ kilo

Kitunguu maji - 2

Tungule/nyanya - 2

Nazi /tui zito - 2 vikombe

Kitunguu saumu(thomu/galic) ilosagwa - 1 kijiko cha supu

Tangawizi mbichi ilosagwa - 1 kijiko cha supu

pilipili shamba/mbichi ilosagwa - kiasi

Mdalasini - 1 kipande

Bizari ya manjano - ½ kijiko cha chai

Bizari ya pilau/jiyrah/cummin - ½ kijiko cha chai

Ndimu/limau - 1

 

Namna Ya Kupika:

Chemsha nyama kwa kutia; chumvi, tangawizi, kitunguu thomu, mdalasini, na bizar zote.

Ipike nyama mpaka iwive na ibakishe supu yake  kidogo.

Changanya tui la nazi pamoja na supu ilobakia.

Panga mbatata katika sufuria.

Tia nyama

Mwagia vitunguu na nyanya ulizotayarisha, tia pilipili.

Mwagia supu ulochanganya na tui

Funika upike mpaka viwive .

Tia ndimu

 

Share