Hadiyth Zisizo Sahihi Kuhusu Swawm Na Ramadhwaan

 

 

Hadiyth Zisizo Sahihi Kuhusu Swawm Na Ramadhwaan

  

www.alhidaaya.com

 

 

 1.

لا تقولوا رمضان، فإن رمضان اسم من أسماء الله تعالى، ولكن قولوا: شهر رمضان

  والحديث موضوع   ترتيب الموضوعات " للذهبي، " الفوائد المجموعة“  للشوكاني

 

“Msiuite  mwezi kwa jina la Ramadhwaan; kwani Ramadhwaan ni jina katika Majina ya Allaah, lakini semeni mwezi wa Ramadhwaan.”

 

Hadiyth hii ni Hadiyth Mawdhwuw’  (ya kutungwa) amezuliwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) imetajwa kwenye kitabu cha Imaam Adh-Dhahabiy cha Hadiyth za kutungwa na kwenye kitabu cha Ash-Shawkaaniy pia kiitwacho Al-Fawaaid.

 

 

2.

أول شهر رمضان رحمة، وأوسطه مغفرة، وأخره عتق من النار

ضعيف أشار ابن خزيمة إلى تضعيفه، وقال الشيخ الألباني: إنه حديث منكر.

 

“Mwanzo wa mwezi wa Ramadhwaan ni rahmah, na katikati yake ni maghfirah, na mwisho wake ni kutolewa kwenye Moto.”

 

Ni Hadiyth Dhwa’iyf; Ibn Khuzaymah ameashiria kuwa ni Hadiyth Dhwa’iyf, na Shaykh Al-Albaaniy amesema ni Hadiyth Munkar.

 

 

3.

صوموا تصحوا

وهو حديث ضعيف ، وإن كان معناه صحيحاً ، وقد ذكره الشيخ الألباني في "ضعيف الجامع الصغير".

“Fungeni mtapata siha (afya).”

 

Ni Hadiyth dhaifu japokuwa maana yake sahihi; ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kwenye kitabu cha Dhwa’iyf Al-Jaami’ Asw-Swaghiyr. 

 

 

4.

لا تزال أمتي بخير ما أخَّروا السحور وعجَّلوا الفطر

رواه أحمد والحديث منكر كما قال الشيخ الألباني،

Ummah wangu utaendelea kuwa katika khayr madhali wanachelewesha Suhuwr (kula daku) na wanaharakisha kufuturu.” [Ameipokea Ahmad na Hadiyth ni Munkar kama alivyosema Shaykh Al-Albaaniy]  

 

 

 

 والصحيح من ذلك حديث:

لَا يَزَالُ النَّاسُ بِخَيْرٍ مَا عَجَّلُوا الْفِطْرَ

Hadiyth iliyo sahihi kuhusu hilo, ni Hadiyth:

“Watu wataendelea kuwa katika khayr madhali watakuwa wanaharakisha kufutari.” [Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

5.

"رجب شهر الله، وشعبان شهري، ورمضان شهر أمتي"

ضعيف ، نص الشيخ الألباني على تضعيفه في السلسلة الضعيفة

“Rajab ni mwezi wa Allaah, na Sha’abaan ni mwezi wangu, na Ramadhwaan ni mwezi wa ummah wangu.”

 

Hadiyth Dhwa’iyf, ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kwenye Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah.

 

 

6.

لو يعلم العباد ما في رمضان لتمنت أمتي أن تكون السنة كلها رمضان...

 موضوع (يعني مكذوب على النبي صلى الله عليه وسلم) قال بذلك ابن الجوزي والألباني وغيرهما. وقال ابن حجر عنه: ضعيف جدا.

 

“Lau wangeelewa waja yaliyomo katika Ramadhwaan, ummah wangu ungalitamani iwe Ramadhwaan mwaka mzima...”

 

Ni Hadiyth Mawdhwuw’ (yaani amezuliwa uongo Rasuli wa Allaah Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema hivyo Ibn Al-Jawzy na Al-Albaaniy na wengineo, na amesema Ibn Hajar kuwa ni Hadiyth dhaifu sana.

 

 

7.

اللهم بارك لنا في رجب وشعبان وبلغنا رمضان

وقد ضعّفه الألباني في "ضعيف الجامع الصغير

 

“Ee Rabb Tubarikie katika Rajab na Sha’abaan na Tubalighishe Ramadhwaan.”

 

Ni Hadiyth Dhwa’iyf ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kwenye kitabu cha Dhwa’iyf Al-Jaami’ Asw-Swaghiyr.

 

 

8.

شعبان شهري، ورمضان شهر الله، وشعبان المطهر، ورمضان المكفر

ضعّفه الألباني في السلسلة الضعيفة.

 

“Sha’abaan ni mwezi wangu, na Ramadhwaan ni mwezi wa Allaah, na Sha’abaan inatwahirisha, na Ramadhwaan inafuta (madhambi).”

 

Ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kuwa ni dhaifu kwenye Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah.

 

 

9.

خمس يفطِّرن الصائم وينقضن الوضوء: الكذب، والنميمة، والغيبة، والنظر بشهوة، واليمين الكاذبة

موضوع. قال ابن أبي حاتم : سألت أبي عن هذا الحديث فقال: هذا حديثُ كَذِبٍ، وقال بوضعه الشيخ الألباني في ضعيف الجامع وليس معنى هذا التساهل في هذه المحرمات ، فإنها تفطر الصائم وتوجب القضاء عند ابن حزم والإمام الأوزاعي (خلافا لجمهور أهل العلم)، وتنقص الأجر بل ربما نسفته عند بقية الأئمة، ولكن المقصود أن نسبة هذا اللفظ إلى النبي صلى الله عليه وسلم لا تجوز.

“Mambo matano yanamfunguza mwenye swawm na yanabatilisha wudhuu: Kusema uongo, kufitinisha, kusengenya, kutazama kwa matamanio, kula yamini ya uongo.”

 

Ni Hadiyth Mawdhwuw’.

 

 

10.

نوم الصائم عبادة"

ضعيف، نص على تضعيفه الألباني في السلسلة الضعيفة

“Usingizi wa mwenye Swawm ni ‘ibaadah.”

 

Ni Hadiyth Dhwa’iyf, amesema hivyo Shaykh Al-Albaaniy kwenye Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah.

 

 

11.

نوم الصائم عبادة، وصمته تسبيح، وعمله مضاعف، ودعاؤه مستجاب، وذنبه مغفور

وهو حديث ضعيف، ذكره الشيخ الألباني في "ضعيف الجامع الصغير".

 

“Usingizi wa mwenye mwenye swawm ni ‘ibaadah, na kunyamaza kwake kimya (kutokusema kwake) ni tasbiyh, na ‘amali yake ni yenye kuongezwa maradufu, na du’aa yake ni yenye kutakabaliwa, na dhambi zake ni zenye kughufuriwa.”

 

Ni Hadiyth Dhwa’iyf ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kwenye kitabu cha Dhwa’iyf Al-Jaami’ Asw-Swaghiyr.

 

 

12.

صائم رمضان في السفر كالمفطر في الحضر

وهو حديث ضعيف، ذكره الشيخ الألباني في "ضعيف الجامع الصغير".

“Mwenye Swawm Ramadhwaan kwenye safari ni sawa asiyefunga hali akiwa mkaazi.”

 

Ni Hadiyth Dhwa’iyf ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kwenye kitabu cha Dhwa’iyful Jaami’ Asw Swaghiyr.

 

 

13.

يوم صومكم يوم نحركم

قال عنه السيوطي في الآلئ : كذب ، لا أصل له. وسبقه إلى ذلك الإمام أحمد بن حنبل كما نقل السخاوي في المقاصد.

 

“Siku ya Swawm yenu (kufunga kwenu) siku ya kuchinja kwenu.”

 

Amesema Imaam As-Suyuutwiy: Hadiyth hii haina asli, na alimtangulia kwa hayo Imaam Ahmad bin Hanbal kama alivyonukuu As-Sakhaawiy kwenye Al-Maqaaswid.

 

 

14.

من أدرك رمضان وعليه من رمضان شيء لم يقضه، فإنه لا يقبل منه حتى يصومه

ذكره الشيخ الألباني في "ضعيف الجامع الصغير".

“Mwenye kukutana na Ramadhwaan huku akiwa ana deni la Ramadhwaan hakulilipa, basi haitokubaliwa Swawm yake mpaka alipe ile anayodaiwa.”

 

Ni Hadiyth Dhwa’iyf ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kwenye kitabu cha Dhwa’iyf Al-Jaami’ Asw-Swaghiyr.

 

 

15.

"يا أيها الناس قد أظلكم شهر عظيم ، شهر فيه ليلة خير من ألف شهر ، جعل الله صيامه فريضة ، وقيام ليله تطوعا ، من تقرب فيه بخصلة من الخير كان كمن أدى فريضة فيما سواه ، ومن أدى فيه فريضة كان كمن أدى سبعين فريضة فيما سواه ، وهو شهر الصبر ، والصبر ثوابه الجنة ، وشهر المواساة ، وشهر يزاد فيه في رزق المؤمن ، ومن فطر فيه صائما كان مغفرة لذنوبه وعتق رقبته من النار ، وكان له مثل أجره من غير أن ينتقص من أجره شيء . قالوا : يا رسول الله ، ليس كلنا يجد ما يفطر الصائم ، قال : يعطي الله هذا الثواب من فطر صائما على مذقة لبن ، أو تمرة ، أو شربة من ماء ، ومن أشبع صائما سقاه الله من الحوض شربة لا يظمأ حتى يدخل الجنة ، وهو شهر أوله رحمة ، ووسطه مغفرة ، وآخره عتق من النار ، فاستكثروا فيه من أربع خصال ، خصلتان ترضون بهما ربكم ، وخصلتان لا غنى بكم عنهما ، أما الخصلتان اللتان ترضون بهما ربكم فشهادة أن لا إله إلا الله ، وتستغفرونه ، وأما الخصلتان اللتان لا غنى بكم عنهما ، فتسألون الجنة ، وتعوذون من النار".

وهو حديث ضعيف لا تقوم به حجة. رواه البيهقي ، وضعفه الألباني في "المشكاة"، وقال: منكر في " السلسلة الضعيفة"

Alitukhutubia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika siku ya mwisho ya mwezi wa Sha’abaan; akasema: "Enyi watu! Umekufikieni mwezi ‘adhimu – na kuna riwaayah nyingine ambayo pia ni ya kutungwa kumeengezwa ‘wenye baraka’ mwezi ndani yake kuna usiku ambao ni bora kuliko miezi elfu; Allaah Amejaalia Swawm yake mwezi huu  kuwa ni fardhi (wajibu), na kisimamo (qiyaam) chake  cha usiku wake ni tatwawwu’u  (kujitolea): sio fardhi wala sio wajibu, atakayejikurubisha ndani yake ndani ya mwezi huu  kwa jambo lolote lile la khayr, basi  jazaa yakehuwa kama mtu aliyetekeleza fardhi katika mwezi mingine usiokuwa huu, na atakayetekeleza fardhi ndani yake ndani ya mwezi huu, basi  jazaa yake huwa kama mtu aliyetekeleza fardhi sabini (70) katika mwezi mingine usiokuwa huu, nao ni mwezi wa Swabr (subira), na subira thawabu yake ni Jannah, na ni mwezi ambao ndani yake riziki ya Muumini huzidishwa, na yeyote yule atakayemfuturisha mwenye swawm ndani yake, basi  jazaa yake itakuwa ni  maghfirah ya madhambi yake, na kuachwa huru shingo yake na Moto, na atapata ujira kama aupatao mwenye swawm bila ya kupungua chochote katika ujira wake mwenye swawm.” Tukasema: Ee Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), sio sote tunaweza kupata cha kumfuturisha huyo mwenye swawm; Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawajibu: "Allaah Humpa thawabu hizi yule atakayemfuturisha mwenye swawm kwa funda la maziwa au kwa kokwa ya tende au kwa funda la maji; na atakayemshibisha mwenye swawm basi Allaah Atamnywesha katika hodhi funda ambalo hatopata kiu baada yake mpaka aingie Jannah; nao ni mwezi ambao mwanzo wake ni rahmah, na katikati yake ni maghfirah, na mwisho wake ni kuachwa huru kutokana na Moto. Na kuna riwaayah nyingine ambayo pia ni ya kutungwa kumeengezwa na atakayempunguzia kazi mtumishi  mfanyakazi wake  ndani ya mwezi huu, Allaah Atamghufuria madhambi yake na kumuacha huru na Moto; basi kithirisheni sana ndani yake mambo manne, mtamridhisha Rabb wenu kwayo na mawili mengine hamjikwasi  hamna budi nayo; ama yale mawili ambayo mtakayoridhisha nayo Rabb wenu ni shahaadah (kushuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah) na mumtake maghfirah, na ama yale mawili mengine ambayo hamna budi nayo ni kuomba Jannah na kujilinda kujikinga kwake na  adhabu  ya Moto."

 

Hadiyth hii ni Dhwa’iyf haiwezi kuwa hoja wala dalili. Ameipokea Al-Bayhaqiyy na akaidhoofisha kwa kusema Dhwa’iyf Shaykh Al-Albaaniy kwenye Al-Mishkaat na akasema ni Hadiyth Munkar kwenye Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah.

 

 

16.

أن امرأتين صامتا وأن رجلاً قال: يا رسول الله إن هاهنا امرأتين قد صامتا وإنهما قد كادتا أن تموتا من العطش فأعرض عنه أو سكت ثم عاد وأراه قال بالهاجرة قال يا نبي الله إنهما والله قد ماتتا أو كادتا أن تموتا قال ادعهما قال فجاءتا قال فجيء بقدح أو عس فقال لإحداهما: قيئي فقاءت قيحاً أو دماً وصديداً ولحماً حتى قاءت نصف القدح ثم قال للأخرى: قيئي فقاءت من قيحٍ ودمٍ وصديدٍ ولحمٍ عبيطٍ وغيره
حتى ملأت القدح ثم قال إن هاتين صامتا عما أحل الله وأفطرتا على ما حرم الله عز وجل عليهما جلست إحداهما إلى الأخرى فجعلتا يأكلان لحوم الناس.

الضعيفة"

“Wanawake wawili walifunga – katika uhai wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kwamba mtu alisema: Ee Rasuli wa Allaah! Hakika wanawake wawili hawa wamefunga na kwamba wao wawili walikaribia kufa kwa kiu; Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)  akampuuza au alinyamaza kimya; kisha – yule mtu  akarejea… akasema: Ee Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)! Hakika wawili hao wamekwisha kufa au wanakaribia kufa – akitafuta wapewe rukhsa ya kufungua kwa hali yao mbaya; Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Waiteni. Akasema: Wakaja wote wawili; akasema: kikaletwa chombo na akaambiwa mmoja wao: Tapika ndani yake yale mliyokuwa mkila. Basi alitapika matapishi au damu na usaha na nyama, alitapika mpaka kile chombo kikajaa nusu yake, na kisha akamwambia yule mwengine wa pili wao: Tapika, basi na yeye alitapika matapishi na damu na usaha na nyama  na mengineo mpaka chombo kikajaa, kisha – Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Hakika wanawake wawili hawa walifunga kwa kujizuilia kutokula  kutokana na yale Aliyoyahalalisha Allaah, na wakafungua Swawm zao  kutokana na yale Aliyowaharamishia Allaah, alikaa mmoja wa wawili hawa kwa mwenzake wakawa wanakula nyama za watu (wanasengenya).”

 

Ni Hadiyth Dhwa’iyf.

 

 

17.

أعطيت أمتي في شهر رمضان خمسا لم يعطهن نبي قبلي أما واحدة ؛ فإنه إذا كان أول ليلة من شهر رمضان ينظر الله
عز وجل إليهم، ومن نظر الله إليه لم يعذبه

وأما الثانية ؛ فإن خلوف أفواههم حين يمسون أطيب عند الله من ريح المسك

وأما الثالثة ؛ فإن الملائكة تستغفر لهم في كل يوم وليلة

وأما الرابعة فإن الله عز وجل يأمر جنته فيقول لها: استعدي وتزيني لعبادي، أوشك أن يستريحوا من تعب الدنيا إلى داري وكرامتي

وأما الخامسة ؛ فإنه إذا كان آخر ليلة غفر الله لهم جميعا
فقال رجل من القوم: أهي ليلة القدر؟ فقال: لا، ألم تر إلى العمال يعملون،
فإذا فرغوا من أعمالهم وفوا أجورهم " وفي لفظ (تستغفر لهم الحيتان

 

ذكره العلامة الألباني في سلسلته الضعيفة وقال في المشكاة فيه هشام ابن أبي هشام ضعيف إتفاقا وهو متروك

 

“Ummah wangu umepewa mambo matano kwenye Ramadhwaan hajapewa Nabiy yeyoye yule kabla yangu; Jambo la kwanza, Unapokuwa usiku wa kwanza kwenye mwezi wa Ramadhwaan Allaah Huwatazama  ummah wangu  na anayetazamwa na Allaah Hatomuadhibu.

Jambo la pili, harufu ya vinywa vyao inapendeza zaidi kwa Allaah kuliko harufu ya miski.

Jambo la tatu, Malaika wanawaombea maghfirah kila siku mchana na usiku.

Jambo la nne, Allaah Huamrisha Jannah Yake kwa kuiambia: Jiandae na jipambe kwa ajili ya waja Wangu, karibu watapumzika kutokana na taabu za dunia na kwenda kwenye Nyumba Yangu na kwenye Karama (utukufu) Yangu.

Jambo la tano, na inapokuwa mwisho wa usiku Allaah Huwaghufuria wote. Akauliza mtu: je, huu ndio usiku wa Laylatul Qadr? – Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Sio; je, huoni kuwa wafanyakazi hufanya kazi na wanapomaliza kazi yao hulipwa ujira wao. Na katika riwaayah: Samaki huwaombea maghfirah.”

 

Ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kuwa ni Dhwa’iyf kwenye Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah na pia akasema kwenye Al-Mishkaat kuwa ndani yake yuko Hishaam bin Abi Hishaam ambaye ni Dhwa’iyf kwa maafikiano na ni Matruwk (aliyeachwa Hadiyth zake).

 

 

18.

إذا كان أول ليلة من شهر رمضان نظر الله عز وجل إلى خلقه، وإذا نظر الله عز وجل إلى عبده لم يعذبه أبدا، ولله عز وجل فى كل ليلة ألف ألف عتيق من النار

موضوع (يعني مكذوب على النبي صلى الله عليه وسلم) قال بذلك ابن الجوزي، والألباني في السلسلة الضعيفة

“Inapokuwa usiku wa mwanzo wa mwezi wa Ramadhwaan Allaah Huwatazama viumbe Wake, na Allaah Anapomtazama mja Wake Hatomuadhibu abadan; na Allaah Huwatoa Motoni katika kila usiku elfu elfu.”

 

Ni Hadiyth Mawdhwuw’ ya kutungwa amezuliwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema hivyo Ibn Al-Jawziy na Al-Albaaniy katika Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah.

 

 

19.

يستقبلكم وتستقبلون ثلاث مرات، فقال عمر بن الخطاب: يا رسول الله وحيٌ نزل؟ قال: لا. قال: عدوٌ حضر؟ قال: لا. قال: فماذا؟ قال عليه الصلاة والسلام: إن الله عز وجل يغفر في أول ليلة من شهر رمضان لكل أهل هذه القبلة.

وقال عنه الألباني: منكر، وذلك في "ضعيف الترغيب والترهيب".

“Atakupokeeni na nyinyi  mtampokea” mara tatu, ‘Umar bin Al-Khattwaab akasema: Ee Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)! Ni Wahyi umeteremshwa? Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  akasema: Sio. ‘Umar bin Al-Khattwaab akasema: Je, ni adui amehudhuria?  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Sio. ‘Umar bin Al-Khattwaab akasema: Basi nini?   Rasuli  wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Hakika Allaah Anawaghufuria katika usiku wa mwanzo wa Ramadhwaan kwa kila mmoja wa katika kabila hili.”

 

Ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kuwa ni Munkar kwenye Dhwa’iyf At-Targhiyb wat-Tarhiyb.

 

 

20.

إن للصائم عند فطره دعوة لا ترد

ضعيف ، أشار إلى ضعفه ابن القيم في زاد المعاد، ونص على تضعيفه الشيخ الألباني في تمام المنة وغيره، وفي الصحيح غنية، 

فقد صح أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال :( ثلاثة لا ترد دعوتهم: الصائم حتى يفطر والإمام العادل ودعوة المظلوم) صححه الألباني في السلسلة الصحيحة ، وشتان بين اللفظين.

“Hakika kwa mwenye Swawm wakati wa kufutari du’aa hairejeshwi (haikataliwi).”

 

Ni Hadiyth Dhwa’iyf, ameashiria hayo Ibn Al-Qayyim kwenye Zaad Al-Ma’aad na pia Shaykh Al-Albaaniy kwenye Tamaam Al-Minnah na na kwengineko, na katika Sahihi kuna zenye kutosheleza, imethibiti kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

“Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“(Watu) watatu du'aa zao hazirudi: Mwenye Swawm hadi afuturu (afutari), Kiongozi muadilifu na du’aa ya aliyedhulumiwa…” [At-Tirmidhiy]

 

Amesema Al-Albaaniy ni Hadiyth Sahihi kwenye Silsilat Al-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah, umbali ulioje baina ya lafdhi mbili hizi.

 

 

21.

كان إذا دخل رمضان شد مئزره ، ثم لم يأتِ فراشه حتى ينسلخ

الحديث ضعَّفه الألباني بهذا اللفظ، قال: والشطر الأول منه صحيح بلفظ: (كان إذا دخل العشر شد مئزره، وأحيا ليلة، وأيقظ أهله) وهو في الصحيحين.

 

“Alikuwa  Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inapoingia Ramadhwaan akikaza shuka yake, kisha hakiendei kitanda chake (halali tena) mpaka Ramadhwaan imalizike”

 

Ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kuwa ni Dhwa’iyf kwa lafdhi hili, na akasema kuwa: Sehemu  nusu  ya pili ya Hadiyth ndio sahihi kwa lafdhi:

 

"Alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) linapoingia kumi la mwisho la Ramadhwaan; alikuwa akikaza shuka yake. Makusudio hapa ni kuwa alikuwa akijibidiisha sana au akijiepusha na wake zake, na akihuisha usiku kwa kufanya ‘ibaadah, na akiamsha ahli zake.” [Al-Bukhaariy]

 

 

22.

أتاكم رمضان، شهر بركة، يغشاكم الله فيه، فينزل الرحمة، ويحط الخطايا ويستجيب فيه الدعاء، وينظر الله تعالى إلى تنافسكم فيه، ويباهي بكم ملائكته، فأروا الله من أنفسكم خيرا،
فإن الشقي من حرم فيه رحمة الله عز وجل

قال الألباني موضوع في تعليقه الترغيب والترهيب

 

“Mmejiwa na mwezi wa Ramadhwaan, mwezi wa baraka, ambao ndani yake Allaah Huwakinga nyinyi, Huteremsha Rahmah Yake, na Husamehe makosa, na Hajibu ndani yake du’aa, na Huangalia ndani yake katika kushindana kwenu katika ufanyaji wa mema na Hujigamba mbele ya Malaika Wake, basi muonyesheni Allaah kutokana na nafsi zenu katika yale yaliyo mazuri, kwa sababu Ash-Shaqiyu (muovu) miongoni mwenu ni yule aliyenyimwa Rahmah za Allaah ('Azza wa Jalla).”

 

Ni Hadiyth Mawdhwuw’ (ya kutungwa), amezuliwa Nabiy Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameitaja Shaykh Al-Albaaniy katika At-Targhiyb wat-Tarhiyb.

 

 

23.

إن الجنة لتزين لرمضان من رأس الحول إلى الحول، فإذا كان أول يوم من رمضان هبّت ريحٌ من تحت العرش، فصفّقت ورق الجنة، فتنظر الحور العين إلى ذلك فيقلن: يا رب اجعل لنا من عبادك في هذا الشهر أزواجاً تقرُّ أعيننا بهم، وتقرّ أعينهم بنا، فما من عبد يصوم يوماً من رمضان إلا زُوّج زوجةً من الحور العين في خيمة من درة مما نعت الله: {حور مقصورات في الخيام} (الرحمن :72)، على كل امرأةٍ سبعون حُلّة ليس منها حلّة على لون الأخرى، تُعطى سبعين لوناً من الطيب ليس منه لونٌ على ريح الآخر، لكل امرأة منهن سبعون ألف وصيفة لحاجتها، وسبعون ألف وصيف، مع كل وصيف صحفةٍ من ذهب، فيها لون طعام تجد لآخر لقمة منها لذة لا تجد لأوله، لكل امرأة منهن سبعون سريراً من ياقوتة حمراء، على كل سرير سبعون فراشاً بطائنها من إستبرق، فوق كل فراش سبعون أريكة، ويُعطى زوجها مثل ذلك على سرير من ياقوت أحمر موشحٍ بالدرّ، عليه سواران من ذهب. هذا بكل يوم صامه من رمضان سوى ما عمل من الحسنات

 ذكره الشوكاني في "الفوائد المجموعة في الأحاديث الموضوعة"

Hakika Jannah hupambwa kwa ajili ya Ramadhwaan kila mwaka, basi inapokuwa siku ya kwanza katika (mwezi wa) Ramadhwaan huvuma upepo chini ya ‘Arsh, majani ya Jannah yakatua mahali pake, na Huwr Al-‘Ayn hutazama hayo na husema: Ee Rabb! Tujaalie kutokana na waja Wako kwenye mwezi huu waume ambao macho yetu yaliwazike nao na macho yao yaliwazike nasi, basi hakuna mja atakayefunga siku katika (mwezi wa) Ramadhwaan isipokuwa ataoa mke kutokana na Al-Huwr Al-‘Ayn kwenye hema la lulu. {{Wanawake wazuri wanaotawishwa katika makhema}} [Ar-Rahmaan: 72]…

Haya ni kwa ajili ya kila siku aliyoifunga katika siku za Ramadhwaan ukitoa yale mema aliyoyafanya.”

 

Ni Hadiyth  Mawdhwuw’ –ya kutungwa, amezuliwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameitaja Ash-Shawkaaniy katika Al-Fawaaid Al-Majmuw’ah fiy Al-Ahaadiyth Al-Mawdhwuw’ah.

 

 

24.

الصَّائم في عبادة من حين يصبح إلى أن يمسي ما لم يغتب؛ فإذا اغتاب خرق صومه.

“Mwenye Swawm huwa yuko kwenye ‘ibaadah kuanzia anapopambazukia mpaka anapoingia usiku madhali hajasengenya; akisengenya tu huharibika Swawm yake.”

 

 

25.

الصَّائم في عبادةٍ من حين يصبح إلى أن يمسي، إذا قام قام، وإذا صلَّى صلَّى، وإذا نام نام، وإذا أحدث أحدث، ما لم يغتب؛ فإذا اغتاب خرق صومه.

“Mwenye kufunga huwa yuko kwenye ‘ibaadah kuanzia anapopambazukia mpaka anapoingia usiku, akisimama husimama, na akiswali huswali, na akilala hulala…”

 

 

26.

اتَّقوا شهر رمضان، فإنَّ الحسنات تضاعف فيه، وكذلك السَّيئات.

“Uogopeni mwezi wa Ramadhwaan, kwani ‘amali njema huzidishwa maradufu ndani yake, na ndio hivyo hivyo kwa ‘amali mbaya.”

 

 

27.

إذا كان أوَّل ليلةٍ من رمضان، فتحت أبواب السَّماء، فلا يغلق منها باب؛ حتى يكون آخر ليلةٍ من رمضان، وليس عبد مؤمن يصلي في ليلة فيها، إلَّا كتب الله له ألفًا وخمسمائة حسنة بكل سجدة، وبني له بيتًا في الجنَّة من ياقوتةٍ حمراء، لها ستون ألف بابٍ، لكل منها قصر من ذهبٍ موشحٍ بياقوتةٍ حمراء، فإذا صام أول يوم من رمضان، غفر له ما تقدم من ذنبه، إلى ذلك اليوم من شهر رمضان، واستغفر له كل يومٍ سبعون ألف ملكٍ، من صلاة الغداة، إلى أن توارى بالحجاب، وكان له بكل سجدة يسجدها في شهر رمضان بليل أو نهار، شجرة يسير الراكب في ظلها خمسمائة عامٍ.

“Inapokuwa usiku wa kwanza katika (mwezi wa) Ramadhwaan, hufunguliwa milango ya mbingu, haufunguki katika hiyo mlango wowote ule mpaka inapokuwa usiku wa mwisho katika (mwezi wa) Ramadhwaan, na haswali mja Muumin yeyote yule katika usiku wowote ule ndani yake isipokuwa Allaah Humuandikia kwa kila sajdah  thawabu ya  mema elfu na mia tano, na Humjengea nyumba katika Jannah…”

 

 

28.

من صلَّى في آخر جمعةٍ من رمضان الخمس الصلوات المفروضة في اليوم والليلة، قضت عنه ما أخل به من صلاة سنته.

“Mwenye kuswali katika (siku ya) Ijumaa ya mwisho kwenye (mwezi wa) Ramadhwaan Swalaah tano za fardhi katika mchana na usiku  Swalaah tano pekee zitamkidhia Swalaah zake zote asizoswali za mwaka wake.”

 

 

29.

من فاتته فرائض ولم يعلم عددها؛ فليصلِّ أربع ركعاتٍ أوَّل جمعةٍ في شعبان، فإن لم يتيسر له ففي أولِّ جمعةٍ من رمضان.

“Mwenye kupitwa na (Swalaah za) fardhi na akawa haelewi idadi yake hizo Swalaah za fardhi asizoziswali  basi na aswali rakaa nne (kwenye siku ya) Ijumaa ya kwanza katika (mwezi wa) Sha’baan, na kama haitokuwa wepesi kwake, basi na aziswali hizo rakaa nne kwenye siku ya Ijumaa ya kwanza katika mwezi wa Ramadhwaan.”

 

 

30.

من قضى صلاةً من الفرائض في آخر جمعةٍ من شهر رمضان، كان ذلك جابرًا لكلِّ صلاةٍ فاتت في عمره إلى سبعين سنةٍ.

“Mwenye kulipa Swalaah  yoyote ile katika (Swalaah za) fardhi katika Ijumaa ya mwisho katika mwezi wa Ramadhwaan, itakuwa ni yenye kitulizo (kisawazishi) kwa kila Swalaah zilizompita katika umri wake mpaka miaka sabini.”

 

 

31.

فضل شهر رجب على الشُّهور، كفضل القرآن على سائر الكلام، وفضل شهر شعبان على الشُّهور، كفضلي على سائر الأنبياء، وفضل شهر رمضان كفضل الله على سائر العباد.

“Ubora wa mwezi wa Rajab kwa miezi mingine ni kama ubora wa Qur-aan kwa maneno mengine, na ubora wa mwezi wa Sha’baan kwa miezi mingine ni kama ubora wangu kwa Manabii wengine, na ubora wa mwezi wa Ramadhwaan ni kama ubora Allaah kwa viumbe.”

 

 

32.

رمضان بالمدينة خيرٌ من رمضان فيما سواه.

“Ramadhwaan (kwenye mji wa) Madiynah ni bora kuliko kwenye mji mwengine wowote usiokuwa Madiynah.”

 

 

33.

رمضان بمكة أفضل من ألف رمضان بغير مكة.

“Ramadhwaan (kwenye mji wa) Makkah ni bora kuliko kwenye mji mwengine wowote usiokuwa Makkah.”

 

 

34.

والَّذي بعثني بالحقِّ نبيًا: إنَّ جبريل أخبرني عن إسرافيل عن الله عزَّ وجلَّ: أنَّ من صلَّى ليلة الفطر مائة ركعةٍ, يقرأ في كلِّ ركعةٍ الحمد لله مرةً, وقل هو الله أحدٌ عشر مراتٍ, ويقول في ركوعه وسجوده عشر مراتٍ: سبحان الله، والحمد لله، ولا إله إلا الله، والله أكبر. فإذا فرغ من صلاته استغفر مائة مرةٍ, ثمَّ يسجد, ثمَّ يقول: يا حيُّ يا قيُّوم يا ذا الجلال والإكرام, يا رحمن الدنيا والآخرة ورحيمهما, يا أرحم الرَّاحمين, يا إله الأولين والآخرين, اغفر لي ذنوبي, وتقبل صومي وصلاتي, والَّذي بعثني بالحقِّ لا يرفع رأسه من السُّجود, حتى يغفر الله له ويتقبل منه شهر رمضان.

“Naapa kwa Yule Aliyenituma kwa haki (nikiwa ni) Nabiy: kwamba Jibriyl ameniambia –kuwa amepokea kutoka kwa – Israafiyl naye amepokea kutoka kwa Allaah ('Azza wa Jalla)  kuwa: Atakayeswali usiku wa Fitwr (usiku wa ‘Iyd) rakaa mia kwa kusoma katika kila rakaa Al-Hamdu LiLLaahi mara moja, na Qul Huwa Allaah mara kumi na moja, na kusema katika rukuu yake na sujudu yake: Subhaana Allaah wal Hamdu LiLLaahi wala ilaaha ila Allaah wa Allaahu Akbar…; naapa kwa Yule Aliyenituma kwa haki hatonyanyua kichwa chake kutoka kwenye sujudu mpaka Allaah Amghufulie na Amtakabalie mwezi wa Ramadhwaan.”

 

35.

انبسطوا في النفقة في شهر رمضان، فإن النفقة فيه كالنفقة في سبيل الله

وهو حديث ضعيف، كما قال الشيخ الألباني في "ضعيف الجامع الصغير" نص على نكارته الألباني في السلسلة الضعيفة.

“Kunjuweni kwenye utoaji katika mwezi wa Ramadhwaan, kwani utoaji ndani yake ni kama utoaji kwenye Njia ya Allaah.”

 

Ni Hadiyth dhaifu kama alivyosema Shaykh Al-Albaaniy kwenye kitabu cha Dhwa’iyf Al-Jaami’ Asw-Swaghiyr na kwenye Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfahamesema kuwa ni Munkar.

 

36.

من أدرك رمضان وعليه من رمضان شيء لم يقضه ، لم يتقبل منه، ومن صام تطوعاً وعليه من رمضان شيء لم يقضه، فإنه لا يتقبل منه حتى يصومه

 والحديث ضعيف، ذكره الشيخ الألباني في "سلسلة الأحاديث الضعيفة".

“Mwenye kukutana na Ramadhwaan huku akiwa ana deni la Ramadhwaan hakulilipa, basi haitokubaliwa kwake, na atayefunga Swawm ya kujitolea (isio za faradhi wala wajibu) huku akiwa ana deni la Ramadhwaan hakulikidhi (hakulilipa) basi haitokubaliwa kwake mpaka kwanza aifunge ile siku anayodaiwa ya Ramadhwaan.”

 

Hadiyth ni Dhwa’iyf. Ameitaja Shaykh Al-Albaaniy kuwa ni dhaifu kwenye Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah.

 

37.

من أفطر يوما من رمضان في غير رخصة رخصها الله له لم يقض عنه صيام الدهر كله وإن صامه

ضعيف، وقد أشار لذلك البخاري وضعفه الألباني في مشكاة المصابيح  

“Mwenye kula siku moja katika Ramadhwaan bila ya rukhsa (udhuru) yoyote ile Aliyoiruhusu Allaah kwake hatoweza kuikidhi (kuilipa funga) ya siku hiyo aliyokula aliyoiacha kwa kutofunga hata kama atafunga dahari.”

 

Ni Hadiyth Dhwa’iyf kama alivyoashiria Al-Bukhaariyy na Shaykh Al-Albaaniy amesema Dhwa’iyf  kwenye Mishkaat Al-Maswaabiyh.

 

 

38.

من اعتكف عشراً في رمضان كان كحجتين وعمرتين

حديث موضوع، ذكره الشيخ الألباني في السلسلة الضعيفة،وضعيف الترغيب والترهيب، وضعيف الجامع الصغير.ويغني عنه ماورد في الصحيح من فضل الاعتكاف في رمضان وخاصة العشر الأواخر منه.

“Mwenye kukaa I’itikaaf siku kumi katika Ramadhwaan huwa jazaa yake kama aliyefanya Hijjah mbili na ‘Umrah mbili.”

 

Ni Hadiyth Mawdhwuw’ (ya kutungwa), amezuliwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameitaja Shaykh Al-Albaaniy katika Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah na Dhwa’iyf At-Targhiyb wat-Tarhiyb na Dhwa’iyf Al-Jaami’ Asw-Swaghiyr.

 

Hakuna haja ya Hadiyth hii kwa kuwa Hadiyth zilizopokewa kwenye vitabu Swahiyh kuhusiana na fadhila za I’tikaaf katika mwezi wa Ramadhwaan na hasa kwenye kumi la mwisho wake zinatosheleza.

 

39.

كان يصلي في شهر رمضان في غير جماعة بعشرين ركعة والوتر

وهو حديث موضوع كما ذكر الشيخ الألباني في السلسلة الضعيفة، وهو خلاف حديث عائشة رضي الله عنها في الصحيحين: ما كان النبي صلى الله عليه وسلم يزيد في رمضان ولا في غيره على إحدى عشرة ركعة.

“Alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiswali kwenye mwezi wa Ramadhwaan si katika Jamaa’ah (akiswali pekee) rakaa ishirini na witr.”

 

Ni Hadiyth Mawdhwuw’ (ya kutungwa), amezuliwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameitaja Shaykh Al-Albaaniy katika Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah nayo ni kinyume na Hadiyth ya Ummul-Muuminiyna ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) iliyo kwenye Swahiyh mbili (Al-Bukhaariy na Muslim) ambayo ni:

 

"Hakuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akizidisha si katika (mwezi wa) Ramadhwaan na wala si katika (miezi) mingine isiyokuwa Ramadhwaan zaidi ya rakaa kumi na moja.” [Al-Bukhaariy]

 

40.

شهر رمضان معلَّق بين السماء والأرض، ولا يرفع إلى الله إلا بزكاة الفطر

"العلل المتناهية" لابن الجوزي، "الضعيفة" للألباني

“Mwezi wa Ramadhwaan huning’inia baina ya mbingu na ardhi, na wala hainyanyuliwi kwa Allaah mpaka kwa Zakaah ya Fitwr.”

 

Ni Hadiyth Dhwa’iyf ameitaja Shaykh Al-Albaaniy katika Silsilat Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah na Ibn Al-Jawziy katika kitabu Al-‘Ilal Al-Mutanaahiyyah.

 

41.

"لو أن الله عز وجل أذن للسماوات والأرض أن تتكلم لبشرت الذي يصوم شهر رمضان بالجنة"

موضوع، ذكره السيوطي في اللآلئ المصنوعة.

“Lau Allaah Angeliidhinisha mbingu na ardhi kusema, basi kama zingeliidhinishwa kusema zingelimbashiria Jannah yule anayefunga mwezi wa Ramadhwaan.”

 

Ni Hadiyth Mawdhwuw’ (ya kutungwa), amezuliwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameitaja As-Suyuutwiy kwenye Al-Laaali Al-Maswnuw’ah.

 

 

 

Share