007 - Swali La 7: Kwa Jambo Gani Waja Wamejua Allaah (سبحانه وتعالى) Anayoyapenda Na Kuyaridhia?

Swali La 7:

 

Kwa Jambo gani waja wamejua Allaah (سبحانه وتعالى) Anayoyapenda na kuyaridhia? (Au vipi waja wamejua yale Anayoyapenda Allaah (سبحانه وتعالى) na kuyaridhia?)

 

Jibu:

 

Wamejua kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kuleta Mitume na kuteremsha vitabu Akiamrisha Anayopenda Allaah, kuyaridhia, kukataza Asiyoyapenda na kuyachukia. Na kwa sababu hiyo, hoja zenye nguvu zilisimama juu yao, na hikmah Yake Allaah (سبحانه وتعالى) ikadhihirika kwa kusema:

 

رُّسُلًا مُّبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى اللَّـهِ حُجَّةٌ بَعْدَ الرُّسُلِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا ﴿١٦٥

Rasuli ni wabashiriaji na waonyaji ili pasikuweko kutoka kwa watu hoja yoyote juu ya Allaah baada ya (kuletwa Rasuli). Na Allaah ni ‘Aziyzan-Hakiymaa (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima).

 

Pia Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

 

قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣١﴾

 Sema (ee Muhammad  صلى الله عليه وآله وسلم): Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufiria - Mwenye kurehemu).

Share