Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) - Salaf Mbora

Salaf Mbora Wa Mwanzo
 
 
Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema kumweleza (bint yake) Faatwimah (Radhwiya Allaahu 'anhaa):
 
 
"Hakika Jibriyl ('Alayhis-Salaam) ana kawaida ya kunisikiliza kisomo changu cha Qur-aan kwa mwaka mara moja.
Na sasa (mwaka huu) amefanya mara mbili, na sioni isipokuwa muda wangu niliyokhitariwa uko karibu.
Kwa hiyo, mche Allaah na kuwa na subira, kwani hakika mimi ni  Salaf bora kwako."
 
 
[Al-Bukhaariy na Muslim]
 
Share