052 - Atw-Twuur
الطُّور
Atw-Twuur: 052
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالطُّورِ ﴿١﴾
1. Naapa kwa mlima.
وَكِتَابٍ مَّسْطُورٍ ﴿٢﴾
2. Na Naapa kwa Kitabu kilichoandikwa.
فِي رَقٍّ مَّنشُورٍ ﴿٣﴾
3. Katika karatasi nyembamba ya ngozi iliyokunjuliwa.
وَالْبَيْتِ الْمَعْمُورِ ﴿٤﴾
4. Na Naapa kwa Nyumba yenye kuamiriwa mara kwa mara (na Malaika).
وَالسَّقْفِ الْمَرْفُوعِ ﴿٥﴾
5. Na Naapa kwa dari iliyonyanyuliwa (mbingu).
وَالْبَحْرِ الْمَسْجُورِ ﴿٦﴾
6. Na Naapa kwa bahari iliyojazwa (maji au itakayowashwa moto).
إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ لَوَاقِعٌ ﴿٧﴾
7. Hakika adhabu ya Rabb wako bila shaka itatokea.
مَّا لَهُ مِن دَافِعٍ ﴿٨﴾
8. Hakuna mzuiaji.
يَوْمَ تَمُورُ السَّمَاءُ مَوْرًا ﴿٩﴾
9. Siku zitakapotaharaki mbingu na kutikisika kikweli.
وَتَسِيرُ الْجِبَالُ سَيْرًا ﴿١٠﴾
10. Na milima ikatembea mwendo wa kasi.
فَوَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿١١﴾
11. Basi ole Siku hiyo kwa wakadhibishao.
الَّذِينَ هُمْ فِي خَوْضٍ يَلْعَبُونَ ﴿١٢﴾
12. Ambao wamo katika kushughulika na upuuzi wakicheza.
يَوْمَ يُدَعُّونَ إِلَىٰ نَارِ جَهَنَّمَ دَعًّا ﴿١٣﴾
13. Siku watakayovurumishwa katika Moto wa Jahannam kwa msukumo wa nguvu.
هَـٰذِهِ النَّارُ الَّتِي كُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ ﴿١٤﴾
14. Huu ndio ule moto ambao mlikuwa mkiukadhibisha.
أَفَسِحْرٌ هَـٰذَا أَمْ أَنتُمْ لَا تُبْصِرُونَ ﴿١٥﴾
15. Je, ni sihiri hii au nyinyi hamuoni?
اصْلَوْهَا فَاصْبِرُوا أَوْ لَا تَصْبِرُوا سَوَاءٌ عَلَيْكُمْ ۖ إِنَّمَا تُجْزَوْنَ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٦﴾
16. Ingieni muungue humo, mkistahmili au msistahmili ni sawasawa kwenu, hakika hapana ila mnalipwa yale mliyokuwa mkiyatenda.
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَنَعِيمٍ ﴿١٧﴾
17. Hakika wenye taqwa watakuwa katika Jannaat na Neema.
فَاكِهِينَ بِمَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ وَوَقَاهُمْ رَبُّهُمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ ﴿١٨﴾
18. Wakifurahia kwa ambayo Amewapa Rabb wao, na Atawalinda na adhabu ya moto uwakao vikali mno.
كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٩﴾
19. Kuleni na kunyweni kwa raha kwa sababu ya mliyokuwa mnatenda.
مُتَّكِئِينَ عَلَىٰ سُرُرٍ مَّصْفُوفَةٍ ۖ وَزَوَّجْنَاهُم بِحُورٍ عِينٍ ﴿٢٠﴾
20. Wakiegemea juu ya makochi ya fakhari yaliyopangwa safusafu, na Tutawaozesha hurulaini: wanawake weupe wazuri wa Jannah wenye macho makubwa ya kupendeza.
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَاتَّبَعَتْهُمْ ذُرِّيَّتُهُم بِإِيمَانٍ أَلْحَقْنَا بِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَمَا أَلَتْنَاهُم مِّنْ عَمَلِهِم مِّن شَيْءٍ ۚ كُلُّ امْرِئٍ بِمَا كَسَبَ رَهِينٌ ﴿٢١﴾
21. Na wale walioamini na wakafuatwa na dhuriya wao kwa Iymaan, Tutawakutanisha nao dhuriya wao na Hatutawapunguzia katika ‘amali zao kitu chochote. Kila mtu atafungika kwa yale aliyoyachuma.
وَأَمْدَدْنَاهُم بِفَاكِهَةٍ وَلَحْمٍ مِّمَّا يَشْتَهُونَ ﴿٢٢﴾
22. Na Tutawapa matunda na nyama katika ambavyo wanatamani.
يَتَنَازَعُونَ فِيهَا كَأْسًا لَّا لَغْوٌ فِيهَا وَلَا تَأْثِيمٌ ﴿٢٣﴾
23. Watabadilishana humo gilasi za mvinyo usiosababisha maneno ya upuuzi wala ya dhambi.
وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ غِلْمَانٌ لَّهُمْ كَأَنَّهُمْ لُؤْلُؤٌ مَّكْنُونٌ ﴿٢٤﴾
24. Na watawazungukia watumishi vijana kwa ajili yao kama kwamba ni lulu zilizohifadhiwa.
وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ ﴿٢٥﴾
25. Na wataelekeana wao kwa wao wakiulizana.
قَالُوا إِنَّا كُنَّا قَبْلُ فِي أَهْلِنَا مُشْفِقِينَ ﴿٢٦﴾
26. Watasema: Hakika sisi tulikuwa kabla tukiishi baina ya ahli zetu huku tukiogopa.
فَمَنَّ اللَّـهُ عَلَيْنَا وَوَقَانَا عَذَابَ السَّمُومِ ﴿٢٧﴾
27. Basi Allaah Akatufadhilisha, na Akatuokoa na adhabu ya moto unaobabua.
إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلُ نَدْعُوهُ ۖ إِنَّهُ هُوَ الْبَرُّ الرَّحِيمُ ﴿٢٨﴾
28. Hakika sisi tulikuwa kabla Tunamuomba Yeye Pekee. Hakika Yeye Ndiye Mwingi wa Ihsani na Fadhila, Mwenye Kurehemu.
فَذَكِّرْ فَمَا أَنتَ بِنِعْمَتِ رَبِّكَ بِكَاهِنٍ وَلَا مَجْنُونٍ ﴿٢٩﴾
29. Basi kumbusha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), kwani hakika wewe kwa Neema ya Rabb wako, si kahini wala si majnuni.
أَمْ يَقُولُونَ شَاعِرٌ نَّتَرَبَّصُ بِهِ رَيْبَ الْمَنُونِ ﴿٣٠﴾
30. Au wanasema (huyu Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ni mshairi, tunamtazamia kupatikana na maafa ya dahari.
قُلْ تَرَبَّصُوا فَإِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُتَرَبِّصِينَ ﴿٣١﴾
31. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Ngojeeni kwani hakika na mimi ni pamoja nanyi ni miongoni mwa wenye kungojea.
أَمْ تَأْمُرُهُمْ أَحْلَامُهُم بِهَـٰذَا ۚ أَمْ هُمْ قَوْمٌ طَاغُونَ ﴿٣٢﴾
32. Au zinawaamrisha akili zao haya? Au basi tu wao ni watu wenye kupindukia mipaka kuasi?
أَمْ يَقُولُونَ تَقَوَّلَهُ ۚ بَل لَّا يُؤْمِنُونَ ﴿٣٣﴾
33. Au wanasema ameibuni (Qur-aan)? Bali hawaamini.
فَلْيَأْتُوا بِحَدِيثٍ مِّثْلِهِ إِن كَانُوا صَادِقِينَ ﴿٣٤﴾
34. Basi walete kauli mfano wake wakiwa ni wakweli.
أَمْ خُلِقُوا مِنْ غَيْرِ شَيْءٍ أَمْ هُمُ الْخَالِقُونَ ﴿٣٥﴾
35. Au wameumbwa pasipo na kitu chochote au wao ndio waumbaji?
أَمْ خَلَقُوا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۚ بَل لَّا يُوقِنُونَ ﴿٣٦﴾
36. Au wameumba mbingu na ardhi? Bali hawana yakini.
أَمْ عِندَهُمْ خَزَائِنُ رَبِّكَ أَمْ هُمُ الْمُصَيْطِرُونَ ﴿٣٧﴾
37. Au wanazo Hazina za Rabb wako, au wao ndio wenye madaraka?
أَمْ لَهُمْ سُلَّمٌ يَسْتَمِعُونَ فِيهِ ۖ فَلْيَأْتِ مُسْتَمِعُهُم بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ ﴿٣٨﴾
38. Au wanazo ngazi wanasikilizia kwa makini humo? Basi msikilizaji wao alete dalili bayana.
أَمْ لَهُ الْبَنَاتُ وَلَكُمُ الْبَنُونَ ﴿٣٩﴾
39. Au (Allaah) Ana mabanati, nanyi mna watoto wa kiume?
أَمْ تَسْأَلُهُمْ أَجْرًا فَهُم مِّن مَّغْرَمٍ مُّثْقَلُونَ ﴿٤٠﴾
40. Au unawaomba ujira kwa hiyo wameelemewa na uzito wa gharama?
أَمْ عِندَهُمُ الْغَيْبُ فَهُمْ يَكْتُبُونَ ﴿٤١﴾
41. Au wanayo ilimu ya ghaibu kisha wao wanaandika?
أَمْ يُرِيدُونَ كَيْدًا ۖ فَالَّذِينَ كَفَرُوا هُمُ الْمَكِيدُونَ ﴿٤٢﴾
42. Au wanakusudia hila? Basi wale waliokufuru wao ndio watakaorudiwa na hila zao.
أَمْ لَهُمْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ اللَّـهِ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٤٣﴾
43. Au wana ilaah asiyekuwa Allaah? Subhaana-Allaah! (Utakasifu ni wa Allaah) kutokana na ambayo wanafanya shirki.
وَإِن يَرَوْا كِسْفًا مِّنَ السَّمَاءِ سَاقِطًا يَقُولُوا سَحَابٌ مَّرْكُومٌ ﴿٤٤﴾
44. Na hata wangeliona pande kutoka mbinguni linaanguka wangelisema: Mawingu yamerundikana.
فَذَرْهُمْ حَتَّىٰ يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي فِيهِ يُصْعَقُونَ ﴿٤٥﴾
45. Basi waachilie mbali mpaka wakutane na Siku yao ambayo humo watapigwa na mngurumo na mwako wa umeme waangamizwe.
يَوْمَ لَا يُغْنِي عَنْهُمْ كَيْدُهُمْ شَيْئًا وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿٤٦﴾
46. Siku ambayo hila zao hazitowafaa kitu chochote, na wala wao hawatonusuriwa.
وَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا عَذَابًا دُونَ ذَٰلِكَ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٤٧﴾
47. Na hakika wale waliodhulumu watapata adhabu nyingine isiyokuwa hiyo, lakini wengi wao hawajui.
وَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ فَإِنَّكَ بِأَعْيُنِنَا ۖ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ حِينَ تَقُومُ ﴿٤٨﴾
48. Na subiri (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa hukumu ya Rabb wako, kwani hakika wewe uko chini ya Macho Yetu. Na Sabbih pamoja na kumhimidi Rabb wako, wakati unapoinuka.
وَمِنَ اللَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَإِدْبَارَ النُّجُومِ ﴿٤٩﴾
49. Na katika usiku Msabbih na zinapokuchwa nyota.
