088- Al-Ghaashiyah

 

 

 

الْغَاشِيَة

Al-Ghaashiyah: 088

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ ﴿١﴾

1. Je, imekujia habari ya tukio la kufunikiza?

 

 

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ خَاشِعَةٌ ﴿٢﴾

2. Nyuso siku hiyo zitadhalilika.

 

 

عَامِلَةٌ نَّاصِبَةٌ ﴿٣﴾

3. Zifanye kazi ngumu na zichoke mno.

 

 

تَصْلَىٰ نَارًا حَامِيَةً ﴿٤﴾

4. Zitaingia moto uwakao vikali na kuungua.

 

 

تُسْقَىٰ مِنْ عَيْنٍ آنِيَةٍ ﴿٥﴾

5. Zitanyweshwa kutoka chemchem yenye kutokota.

 

 

لَّيْسَ لَهُمْ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٍ ﴿٦﴾

6. Hawatokuwa na chakula isipokuwa kutokana na mti wenye miba, wenye kunuka na mchungu mno.

 

 

لَّا يُسْمِنُ وَلَا يُغْنِي مِن جُوعٍ ﴿٧﴾

7. Hakinenepeshi, na wala hakisaidii kuondoa njaa.

 

 

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاعِمَةٌ ﴿٨﴾

8.  Na nyuso (nyingine) Siku hiyo zitakuwa zenye kuneemeka.

 

 

لِّسَعْيِهَا رَاضِيَةٌ ﴿٩﴾

9. Zitafarijika kwa juhudi zake.

 

 

فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ ﴿١٠﴾

10. Kwenye Jannah ya juu.

 

 

لَّا تَسْمَعُ فِيهَا لَاغِيَةً ﴿١١﴾

11. Hazitosikia humo upuuzi wala ubatilifu.

 

 

فِيهَا عَيْنٌ جَارِيَةٌ ﴿١٢﴾

12.  Humo mna chemchem inayobubujika.

 

 

فِيهَا سُرُرٌ مَّرْفُوعَةٌ ﴿١٣﴾

13. Humo mna makochi yaliyoinuliwa.

 

 

وَأَكْوَابٌ مَّوْضُوعَةٌ ﴿١٤﴾

14. Na bilauri zilizopangwa tayari.

 

 

وَنَمَارِقُ مَصْفُوفَةٌ ﴿١٥﴾

15. Na matakia yaliyopangwa safusafu.

 

 

وَزَرَابِيُّ مَبْثُوثَةٌ ﴿١٦﴾

16. Na mazulia yaliyopambwa na ya fahari yaliyotandazwa.

 

 

أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى الْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ ﴿١٧﴾

17. Je, hawawataamuli ngamia namna walivyoumbwa?

 

 

وَإِلَى السَّمَاءِ كَيْفَ رُفِعَتْ ﴿١٨﴾

18. Na mbingu vipi zilivyonyanyuliwa?

 

 

وَإِلَى الْجِبَالِ كَيْفَ نُصِبَتْ ﴿١٩﴾

19. Na milima vipi imekongomewa imara kabisa?

 

 

 

وَإِلَى الْأَرْضِ كَيْفَ سُطِحَتْ ﴿٢٠﴾

20. Na ardhi vipi ilivyotandazwa?

 

 

فَذَكِّرْ إِنَّمَا أَنتَ مُذَكِّرٌ ﴿٢١﴾

21. Basi kumbusha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Hakika wewe ni mkumbushaji tu.

 

 

لَّسْتَ عَلَيْهِم بِمُصَيْطِرٍ ﴿٢٢﴾

22. Wewe si mwenye kuwadhibiti.

 

 

إِلَّا مَن تَوَلَّىٰ وَكَفَرَ ﴿٢٣﴾

23. Isipokuwa yule atayegeuka na akakufuru.

 

 

فَيُعَذِّبُهُ اللَّـهُ الْعَذَابَ الْأَكْبَرَ ﴿٢٤﴾

24. Basi huyo Allaah Atamuadhibu adhabu kubwa kabisa.

 

 

إِنَّ إِلَيْنَا إِيَابَهُمْ ﴿٢٥﴾

25. Hakika Kwetu ndio marejeo yao.

 

 

ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا حِسَابَهُم ﴿٢٦﴾

26. Kisha bila shaka ni juu Yetu hesabu yao.

 

 

 

 

Share