087 - Al-A'laa
الْأَعْلَى
087-Al-A’laa
087-Al-A’laa: Utangulizi Wa Suwrah
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى ﴿١﴾
1. Sabbih Jina la Rabb wako Mwenye ‘Uluwa Aliyetukuka kabisa kuliko vyote.[1]
الَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ ﴿٢﴾
2. Ambaye Ameumba (kila kitu) kisha Akasawazisha.
وَالَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ ﴿٣﴾
3. Na Ambaye Amekadiria na Akaongoza.
وَالَّذِي أَخْرَجَ الْمَرْعَىٰ ﴿٤﴾
4. Na Ambaye Ametoa malisho.
فَجَعَلَهُ غُثَاءً أَحْوَىٰ ﴿٥﴾
5. Kisha Akayafanya majani makavu, meusi.
سَنُقْرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰ ﴿٦﴾
6. Tutakufanya uisome (Qur-aan ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kisha hutoisahau.
إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُۚ إِنَّهُ يَعْلَمُ الْجَهْرَ وَمَا يَخْفَىٰ ﴿٧﴾
7. Isipokuwa yale Ayatakayo Allaah. Hakika Yeye Anayajua ya jahara na yale yanayofichikana.
وَنُيَسِّرُكَ لِلْيُسْرَىٰ ﴿٨﴾
8. Na Tutakuwepesishia kwa yaliyo mepesi.
فَذَكِّرْ إِن نَّفَعَتِ الذِّكْرَىٰ ﴿٩﴾
9. Basi kumbusha ikiwa unafaa ukumbusho.
سَيَذَّكَّرُ مَن يَخْشَىٰ ﴿١٠﴾
10. Atakumbuka yule anayeogopa.
وَيَتَجَنَّبُهَا الْأَشْقَى ﴿١١﴾
11. Na atajiepusha nao fedhuli.
الَّذِي يَصْلَى النَّارَ الْكُبْرَىٰ ﴿١٢﴾
12. Ambaye atauingia moto mkubwa kabisa na kuungua.
ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَىٰ ﴿١٣﴾
13. Kisha hatokufa humo, na wala hatokuwa na uhai (wa raha).
قَدْ أَفْلَحَ مَن تَزَكَّىٰ ﴿١٤﴾
14. Hakika amefaulu ambaye amejitakasa.
وَذَكَرَ اسْمَ رَبِّهِ فَصَلَّىٰ ﴿١٥﴾
15. Na akadhukuru Jina la Rabb wake na akaswali.
بَلْ تُؤْثِرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا ﴿١٦﴾
16. Bali mnahiari zaidi uhai wa dunia.
وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ ﴿١٧﴾
17. Na hali Aakhirah ni bora zaidi na ya kudumu zaidi.
إِنَّ هَـٰذَا لَفِي الصُّحُفِ الْأُولَىٰ ﴿١٨﴾
18. Hakika haya bila shaka yamo katika Suhuf (Maandiko Matukufu) ya awali.[2]
صُحُفِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ ﴿١٩﴾
19. Suhuf ya Ibraahiym na Muwsaa.
