095 - At-Tiyn

 

  التِّين

 

095-At-Tiyn

 

095-At-Tiyn: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

وَالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ ﴿١﴾

1. Naapa kwa tini na zaytuni.[1]

 

 

 

وَطُورِ سِينِينَ ﴿٢﴾

2. Na Naapa kwa Mlima wa Sinai.

 

 

 

وَهَـٰذَا الْبَلَدِ الْأَمِينِ ﴿٣﴾

3. Na Naapa kwa mji huu wa amani (Makkah).[2]

 

 

 

لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ فِي أَحْسَنِ تَقْوِيمٍ ﴿٤﴾

4. Kwa yakini Tumemuumba binaadam katika umbile bora kabisa.[3]

 

 

 

ثُمَّ رَدَدْنَاهُ أَسْفَلَ سَافِلِينَ ﴿٥﴾

5. Kisha Tukamrudisha chini kabisa (motoni) ya walio chini.

 

 

 

إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَلَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ ﴿٦﴾

6. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema; hao watapata ujira usiokatika.

 

 

 

فَمَا يُكَذِّبُكَ بَعْدُ بِالدِّينِ ﴿٧﴾

7. Basi lipi baada ya yote hayo linakufanya ukadhibishe (Siku ya) malipo?!  

 

 

 

 

أَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَحْكَمِ الْحَاكِمِينَ ﴿٨﴾

8. Je, kwani Allaah Si Mwadilifu zaidi kuliko mahakimu wote?  

 

 

 

[1] Allaah Anaapia Tiyn Na Zaytuni:

 

Allaah (عزّ وجلّ) Anaapia miti miwili hiyo kutokana na manufaa yake mengi pamoja na matunda yake, na pia kutokana na kuwa ndio kilimo kikuu kinachoongoza katika ardhi ya Sham mahali pa Nabiy ‘Iysaa mwana wa Maryam (عليه السّلام). [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

[2] Utukufu Wa Makkah Na Fadhila Zake:

 

Rejea Al-Balad (90:1) na Al-An’aam (6:92) kwenye faida kuhusu utukufu wa Makkah na Fadhila zake.

 

[3] Binaadam Ameumbwa Katika Umbo Bora Kabisa:

 

Rejea Al-Infitwaar (82:7-8) kwenye faida na Rejea mbalimbali.

 

 

 

Share