100 - Al-'Aadiyaat

  الْعَادِيَات

Al-‘Adiyaat: 100

 

(Makkiyyah)

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

وَالْعَادِيَاتِ ضَبْحًا ﴿١﴾

1. Naapa kwa farasi waendao mbio mno wakipumua.

 

 

فَالْمُورِيَاتِ قَدْحًا ﴿٢﴾

2. Kisha Naapa kwa wenye kutoa cheche za moto (kwa msuguano wa kwato zao chini.)

 

فَالْمُغِيرَاتِ صُبْحًا ﴿٣﴾

3. Wenye kushambulia asubuhi.

 

 

فَأَثَرْنَ بِهِ نَقْعًا ﴿٤﴾

4. Huku wakitimua wingu la vumbi kubwa 

 

 

فَوَسَطْنَ بِهِ جَمْعًا ﴿٥﴾

5. Kisha wakapenya katikati (ya maadui) wote.

 

 

إِنَّ الْإِنسَانَ لِرَبِّهِ لَكَنُودٌ ﴿٦﴾

6. Hakika mwana Aadam kwa Rabb wake bila shaka ni mtovu wa shukurani.

 

 

وَإِنَّهُ عَلَىٰ ذَٰلِكَ لَشَهِيدٌ ﴿٧﴾

7. Na hakika yeye juu ya hayo bila shaka ni shahidi.

 

 

وَإِنَّهُ لِحُبِّ الْخَيْرِ لَشَدِيدٌ ﴿٨﴾

8. Na hakika yeye ni mwingi mno wa kupenda mali.

 

أَفَلَا يَعْلَمُ إِذَا بُعْثِرَ مَا فِي الْقُبُورِ ﴿٩﴾

9. Je, hajui yatakapopinduliwa juu chini na kufichuliwa vile vilivyomo kaburini?

 

 

وَحُصِّلَ مَا فِي الصُّدُورِ ﴿١٠﴾

10. Na yatapodhihirishwa yale yaliyomo vifuani?

 

 

إِنَّ رَبَّهُم بِهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّخَبِيرٌ ﴿١١﴾

11. Hakika Rabb wao Siku hiyo kwao, bila shaka ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.

 

 

Share