109 - Al-Kaafiruwn
الْكَافِرُون
Al-Kaafiruwn: 109
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ ﴿١﴾
1. Sema: Enyi makafiri!
لَا أَعْبُدُ مَا تَعْبُدُونَ ﴿٢﴾
2. Siabudu yale mnayoyaabudu sasa.
وَلَا أَنتُمْ عَابِدُونَ مَا أَعْبُدُ ﴿٣﴾
3. Na wala nyinyi hamtoabudu Yule ninayemwabudu sasa.
وَلَا أَنَا عَابِدٌ مَّا عَبَدتُّمْ ﴿٤﴾
4. Na wala mimi sitoabudu yale mliyoyaabudu nyuma.
وَلَا أَنتُمْ عَابِدُونَ مَا أَعْبُدُ ﴿٥﴾
5. Na wala nyinyi hamtoabudu Yule Ninayemwabudu.
لَكُمْ دِينُكُمْ وَلِيَ دِينِ ﴿٦﴾
6. Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.
