Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Khatwiyb Kusema "Kimu Swalaah" Baada Ya Khutwbah Ya Ijumaa

 

Hukmu Ya Khatwiyb Kusema "Kimu Swalaah" Baada ya Khutbah Ya Ijumaa

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Aliulizwa Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) kuhusiana na kauli ya Khatwiyb, "Na Kimu Swalaah", je, hili limepokewa kutoka kwa Salaf (Wema waliotangulia)?

 

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) akajibu:

 

Sijui hili kama limepokelewa kutoka kwa  Salaf; nakusudia kauli ya Khatwiyb anapomaliza Khutbah, kusema, "Kimu Swalaah, hakika Swalaah hukataza yaliyo machafu na maovu".

 

Haimpasi Imaam kusema maneno haya, bali anapomaliza Khutbah, anashuka (kutoka katika Minbar) na kisha hukimiwa Swalaah kama alivyokuwa akifanya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Makhaliyfah wake waongofu.

 

Na ama hii nyongeza, haikupokelewa kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), wala kutoka kwa Makhaliyfah wake waongofu, wala kutoka kwa mmoja wa Maimaam; na kwa hali hiyo, hakika hukatazwa neno hilo.

 

[Fataawa Nuur 'Alaa Ad-Darb]

 

 

 

Share