Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Kosa Kusema “Nımefanya Juhudi Kubwa, Mengineyo Namwachia Allaah”

Kosa Kusema “Nımefanya Juhudi Kubwa, Mengineyo Namwachia Allaah”

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn  (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

 SWALI: 

 

Ni usahihi wa kusema: “Nımefanya Juhudi Kubwa, Mengineyo Namwachia Allaah?”

 

 

JIBU:

 

“Kauli hiyo haifai kwa sababu ina maanisha kuwa  mtendaji aliitegemea nafsi yake kwanza:

 

Ama kauli: “Nimefanya juhudi kubwa na namuomba Allaah Anisaidie.” Kauli hii ni inafaa. Ama ile ya mwanzo: “Nimefanya juhudi kubwa na mengine namwachia Allaah.”  Huenda anayesema hivyo  ana maana ya kuwa yale ambayo nimeweza kuyafanya nimeyafanya na yale ambayo siyawezi namwachia Allaah. Hata hivyo asili ya maneno haya ni makosa. Bali anatakiwa aseme: “Nimefanya juhudi kubwa na namuomba Allaah Anisaidie”

 

[Fatwa ya Shaykh Muhammad bin ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)  katika jarida la Al-Hisba, toleo la 50 uk 17]

 

Share