Utengenezaji Wa Caramel Au Tofi Kwa Maziwa Mazito

Utengenezaji Wa Caramel Au Tofi Kwa Maziwa Mazito

Vipimo

Maziwa mazito (condensed milk) - 1 kibati cha 395 gm

Cream ya vibati - 2 vidogo vya 170 gms

Sukari - 1 kikombe

Siagi -3 vijiko vya kulia   

Maziwa - ¼ kikombe    

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1-Changanya vitu vyote katika sufuria isipokuwa maziwa. Weka katika moto.

2-Iache ichemke, huku unakoroga usiachie mkono mpaka ibadilike rangi iwe hudhurungi au brown kiasi upendavyo.

3-Epua, Changanya na siagi, na  na maziwa utazame kiasi upendacho cha uzito.

4-Iache ipowe kisha ihifadhi katika chupa ya gilasi.

 

Kidokezo:

1-Unaweza kutengeneza zaidi ya mara moja yake ukitaka kuhifadhi nyingi katika chupa kutumilia katika vitamu kama kaimati, keki, biskuti na kadhaalika.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

Share