Kaimati Za Shira Ya Tende

VIPIMO
Unga 2 vikombe
Hamira 1 Kijiko cha chai
Samli imoto 2 Kijiko vya Supu
Maziwa au Tui la nazi 1 ½ Kikombe cha chai (inategemea kikombe)
Mafuta ya kukaangia Kiasi
Shira ya Tende (Ya Tayari) Kiasi
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1) Pasha Samli iwe moto kabisa.
2) Changanya unga Hamira, Samli, Maziwa Au Tui la nazi kisha
vuruga
3) Ukiuumuka (ukifura) choma kaimati katika mafuta ya moto
kawaida ya kuchoma kaimati.
4) Ziepue na zichuje mafuta.
5) Zitie katika bakuli au sahani na mwagia Shira ya Tende kiasi
upendavyo. Tayari kuliwa.
Kidokezo: Unaweza kutumia shira ya kawaida ukipenda badala ya tende
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


