Shaykh Swaalih Al-Fawzaan - Si Kila Anayedai Usalafi Ni Salafi

Si Kila Anayedai Usalafi Ni Salafi

Shaykh Swaalih Al-Fawzaan

www.alhidaaya.com

 

Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) amesema:

 

“Si kila anayedai Usalafi, anakuwa (Salafi).

Wameudai (Usalafi) watu (Wajinga) wasiojua Manhaj ya Salafi.

Na wakadai (Usalafi) watu (wanaopiga vita) wanaojihusisha na Manhaj ya Khawaarij kwa kumwaga damu na kuleta ufisadi ardhini.

Na wakadai (Usalafi) watu (wanaojidai wana elimu) ambao hawajachukua elimu kutoka kwa ‘Ulamaa, bali wamechukua kutoka kwenye vitabu na kujisomea na kuhifadhi Nuswuwsw (maandiko) kwa ufahamu tu (binafsi).

 

Na Allaah (Subhaanahu) Anasema:

{{Na wale waliotangulia awali (katika Uislamu) miongoni mwa Muhaajiriyn (wa Makkah), na Answaar (wa Madiynah), na wale waliowafuata kwa ihsaan…}} (Kwa ihsaan) yaani: kwa itqaan (usahihi, ufanisi)

 

[Haqiyqatu Al-Manhaj As-Salafiy, uk. 65]

 

 

Share